1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yashinikiza vikwazo zaidi dhidi ya Iran

23 Februari 2008
https://p.dw.com/p/DC7q

WASHINGTON:

Marekani inashinikiza kuiwekea Iran vikwazo zaidi,kufuatia ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la Nishati ya Nyuklia la Umoja wa Mataifa-IAEA.Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani,Condoleezza Rice amesema,ripoti hiyo mpya ni sababu ya kutosha kupitisha azimio la tatu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Uingereza na Ufaransa zilipendekeza mswada wa azimio hilo siku ya Alkhamisi katika Baraza la Usalama.

Ripoti iliyotolewa siku ya Ijumaa na mkuu wa IAEA bwana Mohamed El-Baradei, imeituhumu Iran kuwa bado haijaeleza kikamilifu kuhusu mradi wake wa nyuklia na vile vile inaendelea kurutubisha uranium.Nchi za Magharibi zinaituhumu Iran kuwa inajaribu kutengeneza silaha za nyuklia kwa siri,kwa kutumia mradi wake wa nishati ya nyuklia.Serikali ya Iran lakini inakanusha tuhuma hizo.