1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yatangaza mapendekezo ya kukabiliana na nakisi

Admin.WagnerD14 Aprili 2011

Rais Barack Obama wa Marekani ametangaza mapendekezo ya kupunguza nakisi ya bajeti ya Marekani kwa kiasi cha dola trilioni 4 kwa kipindi cha miaka 12, ikiwa ni katika juhudi za kukabiliana na msukosuko wa kiuchumi nchini

https://p.dw.com/p/10tOT
Rais wa Marekani, Barack ObamaPicha: AP

Baada ya tangazo hilo, Chama cha Republican kinasema hatua hiyo ya Obama ni ya kisiasa hasa ikizingatiwa kuwa uchaguzi wanukia. Wakosoaji wanasema Obama ameshindwa kudhibti tatizo la nakisi ya bajeti ya  nchi hiyo.

Obama anajaribu kuelezea mpango wake huo ikiwa ni mara ya kwanza kuzungumza tangu atangaze kuwania tena kushiriki kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2012.

Upungufu wa kiasi cha trilioni 1.4 katika bajeti ya kwa mwaka, umekuwa mzigo mkubwa kwa Wamarekani wengi. Obama amekuwa katika jitihada ya kukabilana na tatitizo hilo wakati Wizara ya Fedha ya Marekani ikikiona kiasi hicho, kuwa kikubwa kuliko kilivyotarajiwa.

Hisa za makampuni ya silaha zilianguka baada ya Obama kupunguza bajeti ya Wizara ya Ulinzi.  Hisa za makapuni zitatwaja kufikia asilimia 1.6.

Huku akitoa wito wa kutaka majadiliano zaidi na chama cha Republican kuhusu kupunguza matumizi, Obama alitumia muda mwingi hotuba yake kuzungumzia mipango ya serikali katika sekta ya afya na kupunguza kodi kwa watu wa kawaida na wafanaybiashara wa kati.

Akizungumzia mapendekezo ya Republican,Obama amesema hakuna jambo lolete la msingi zaidi madai ya kupungusa nakisi ya bajeti kw kukata kodi kwa mamilionea na mabilionea.

Katika hotuba yake hiyo alioiwasilisha katika ukumbi wa chuo kikuu cha George Washington amesema atatenga fungu la kiasi cha dola bilioni 480 kwa ajili ya madawa na misaada ya madawa, mpango wa kusadia wazee na masikini.

Kwa upande wao Republican wanasema hotuba ya Obama inaonesha dhahiri kwamba hayupo makini na nakisi ya bajeti.Wamesema mapendekezo aliyoyatoa hayatatatua tatizo badala yake yatavuruga uchumi wa nchi.

Wanasema kinachofanyika ni kwamba wasaidizi wake wanataka kumuonesha Obama kuwa ni kiongozi katika vyama vya visiana katika mjadala wa bajeti na kuongeza kwamba hotuba hiyo iliwalenga wapiga kura.

Norman Ornstei, Msomi kutoka Tasisi ya Ujasiriali ya Marekani, amesema hotuba hiyo ilikuwa na shabaha ya kukosoa mpango uliwasilisha na Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti wa Bunge la Marekani Paul Ryan aliyowasilisha siku chache zilizopita.

Hata hivyo republicana imekwisha sema kwama haitapigia kura mapendekezo hayo.Mbunge mwingine kutoka Republican Jonh Boehner amesema mapngo wa Obama ambao unajumuisha kupanda kwa kodi si mwanzo mzuri.

Mwandishí: Sudi Mnette/Reuters

Mhariri: Abdul-Rahman