1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marion Jones arudisha medali

Ramadhan Ali9 Oktoba 2007

Bingwa wa olimpik na malkia wa mbio fupi Marion Jones wa Marekani amekabidhi leo medali 5 za Olimpik alizoshinda Sydney,Australia,2000.

https://p.dw.com/p/C7nV

Malkia wa mbio fupi aliejifedhehi Marion Jones wa Marekani,amekabidhi kwa hiyari yake hii leo medali zake 5 za Olympik alizoshinda Sydney.Australia,2000 na amekubali marufuku ya miaka 2 katika medani ya riadha.

Mkasa wa mchezaji dimba wa timu ya taifa ya Ujerumani chini ya umri wa miaka 21 wa asili ya ki-iran kukataa kwenda na timu yake Israel,kumezusha malalamiko makali kutoka Baraza la wayahudi la Ujerumani na kura imepigwa leo kwa duru ijayo ya kombe la Ulaya la UEFA.

Marion Jones sibingwa tena wa olimpik.Binafsi amerejesha hii leo medali zake zote 5 -3 za dhahabu na 2 za shaba alizoshinda katika michezo ya Olimpik ya mwaka 2000 huko sydney Australia.

Isitoshe, malkia huyo wa zamani wa mbio fupi amekubali marufuku ya kutoshiriki mashindanoni kwa muda wa miaka 2.Ijumaa iliopita aliungama hadharani na mahkamani kwamba akitumia madawa kabla michezo ya Olimpik ya 2000.Medali hizo 5 zilikabidhiwa leo kamati ya Olimpik ya marekani a