1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marseille, Ufaransa. Ufaransa yaadhimisha mwaka mmoja baada ya ghasia.

29 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCyC

Mwanamke mmoja amepata majeraha ya kuungua kwa moto wakati watu waliokuwa wakifanya ghasia walipochoma moto basi ambalo alikuwa akisafiria katika mji wa kusini wa Marseille.

Polisi wamesema abiria wengine watatu wametibiwa kutokana na kuvuta hewa ya moshi.

Shambulio hilo lilitokea wakati Ufaransa unaadhimisha mwaka wa kwanza tangu kutokea ghasia ambazo zimewaathiri wengi wa watu wanaoishi katika maeneo ya masikini nchini humo, ambayo yanaishi zaidi wahamiaji.

Wahuni wamechoma moto takriban mabasi sita katika vitongoi kuzunguka mji wa Paris katika wiki moja iliyopita katika hali ya kuzuka tena kwa ghasia kabla ya maadhimisho hayo, lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa katika matukio hayo.