1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MASERU: Uchaguzi wa bunge nchini Lesotho

17 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCRP

Wapiga kura katika Ufalme wa Lesotho hii leo wanapiga kura kuchagua bunge lenye viti 120. Kutoka jumla ya wakazi milioni 1.8 wa dola hilo dogo linalozungukwa na Afrika ya Kusini,ni kiasi ya watu 900,000 waliokuwa na haki ya kupiga kura. Uchaguzi huo,unatazamiwa kuwa mashindano makali kati ya chama tawala cha “Lesotho Congress for Democracy“ cha waziri mkuu Pakalitha Mosisili na chama kilichoundwa hivi karibuni “All Basotho Congress“ kinachoongozwa na waziri wa nje wa zamani,Tom Thabane.Upinzani umeituhumu serikali kuwa imeshindwa kupunguza umasikini na kuleta maendeleo ya kimsingi.