1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashabiki 13 wauwawa Kongo

15 Septemba 2008

Machafuko yalizuka uwanjani huko Kivu ya mashariki pale timu 2 zilipokutana .

https://p.dw.com/p/FIed
Luca Toni atia mabao 2.Picha: picture-alliance /dpa

Sepp Blatter,Rais wa FIFA asema kombe lijalo la dunia halitaaniwa kwengineko bali Afrika kusini -

Licha ya mabingwa Bayern Munich kuondoka na pointi 3 mjini Cologne,ni Hamburg inayoongoza orodha ya Bundesliga na huko Kongo mashabiki kadhaa wauwawa uwanjani-kisa nini ? tutawafungulia pia pazia la changamoto ya Septemba 26 kati ya mahasimu 2 wa jadi Yanga na simba nchini Tanzania.

►◄

Katika Liogi mashuhuri za Ulaya, hannover jana ilikomesha kiu chake cha mapambano 3 bila ya kutia magoli ilipoizaba Borussia Monschengladbach mabao 5-1 na kujikomboa kutoka safu ya chini kabisa ya ngazi ya Bundesliga.

Bochum pia ilijipatia ushindi wake wa kwanuza msimu huu mpya ilipoikomea Armenia Bielefeld mabao 2-0 matokeo ambayo yameiwacha Bielefeld timu ya pili kutoka mkaini mwa Buindesliga ikiwa na pointi 2 tu-1 kuliko Energie Cottbus inayoburura mkia.

Baada ya mechi 4 za msimu huu mpya,Hamburg inaongoza orodha ya Ligi ikiwa na jumla ya pointi 10 kufuatia ushindi wake wa mabao 3-2 dhidi ya Bayer Leverkusen hapo jumamosi.

Mabingwa Bayern munich walioizaba FC Cologne mabao 3:0 hapo jumamosi wameparamia ngazi hadi nafasi ya pili wakiwa sasa na pointi 8.

Mpambano wao mjini Cologne hapo jumamosi uligubikwa na shangwe za mashabiki wa Cologne kwa stadi wao wa zamani Lukas Podolski anaeichezea sasa Bayern Munich lakini haridhiki kwa kutochezeshwa tangu mwanzo.

Hata dhidi ya klabu yake ya zamani,Podolski aliteremshwa uwanjani kipindi cha pili .Ilikua yeyxe alietayarisha bao la pili la Luca Toni kabla mnamo dakika ya 90 ya mchezo,mwenyewe Podolski kusindikiza bao la 3 la Munich katika lango la klabu yake ya zamani.

hii iliwagawa mashabiki wa Fc Cologne:Kuna wale waliomshangiria kwa kutia bao langoni mwa klabu yake ya zamani na kuna wale waliokasirika kwanini ameshangiriwa.

FC Cologne, kitambo sasa ikidai Podolski arudi Cologne kwavile haridhiki n a hali ya mambo kwa mabingwa Bayern Munich.

Kuhusu jinsi alivyoshangirwa uwanjani mjini Cologne hapo jumamosi, kocha wa Bayern Munich Jurgen klinsmann alielezea anafahamu kuwa Podolski anapendwa mjini Cologne lakini wacologne watambue ni mchezaji wa Bayern Munich wakati huu na ataendelea kuwa hivyo:

"Ni kijana wa Cologne na ni jambo la kufurahisha sana kwua ni hivyo.Ni barabara kabisa jinsi anavyoshangiriwa lakini,Lukas anabidi kufuata njia yake huku kwetu na atafuata njia hiyo."

Alisema kocha wa Bayern Munich ,Jurgen klinsmann.

Ama katika Premier League-Ligi ya Uingereza,Manchester united ilikiona cha mtema kuni ilipotandikwa mabao 2:1 na FC Liverpool.Fulham pia ikatamba kwa mabao 2:1 mbele yaBolton Wanderers.Arsenal lakini ilinguruma kama simba kweli mbele ya Blackburn Rovers kwa mabao 4:1.Wigan Athletic bao 1 na Sunderland 1-Portsmouth lakini ilinguruma mbele ya Middlesbrough ilipoichapa mabao 2:1.

West Bromwiich Albion imeichapa Westham United 3-2.

Kileleni mwa Ligi inaongoza Chelsea ilioizaba Manchester City mabao 3-2.

Liverpool inafuata nafasi ya pili ikiwa opia na pointi 10 sawa na Chelsea.Arsenal inanyatia nafasi ya 3 ikiwa pointi 1 nyuma.

katika la Liga-Ligi ya Spian Espanyol imeparamia kileleni kwa bao la dakika za mwisho jana katika lango la Recreativo Huelva.Alikua Luis Aarcia alielifumania lango la huelva kama alivyofanya dhidi ya Valladolid wiki 2 nyuma.

Jana Getafe ailiondoka sare 0:0 na Betis wakati Villareal ilikumta Depotivo La Coruna bao 1:0.

Mpambano kati ya Real Madrid na Numancia ulimalizika kwa ushindi wa Real wa mabao 4-3.Real sasa imeangukia nafasi ya 8 ya ngazi ya Ligi.Valencia inaifuata Espanyol iko klileleni mwa Ligi.

katika serie A, Ligi ya Itali,AC Milan ilipatwa na pigo la pili mwishoni mwa wiki ilipozabwa mabao 2:0 na Genoa.Licha ya vishindo vikubwa vya mastadi wa Milan akina Kaka,Ronaldinho na Andry Shevchenko,Genoa ilitamba.Siena ilishinda mabao 2:0 dhidi ya Cagliari wakati Reggina na Torino zilimudu sare bao 1:11.Bao la mbrazil Amauri lilitosha kuipa Juventus jana ushindi dhidi ya Udinese.mabingwa Inter milan waliitimua Catania mabao 2:1 jumamosi licha ya kucheza na wachezaji 10 uwanjani.Palermo ilitoka nyuma na mwishoe kuizaba Roma mabao 3-1.

Lazio Toma na Bergamo kila moja ikiwa na pointi 6 zaongoza Serie A.

Hakuna shaka shaka tena kuwa kombe lijalo la dunia la dimba, halitachezwa Afrika kusini.Rais wa FIFA-shirikisho la kabumbu ulimwenguni Sepp Blatter

akiwa Pretoria,Afrika kusini mwoshoni mwa wiki aliihakikishia kuwa FIFA iko nyuma yake kikamilifu kuandaa kombe la dunia kwa ufanisi 2010.

Alisema hayo baada ya mkutano wake na rais Thbao Mbeki akianza ziara yake ya siku 4 nchni.

Akiwageukia wakosoaji,Blatter alisema na ninamnukulu,

""Wanapaswa kuungama kwamba viwanja vitakuwa tayari na wageni watapokewa vyema na kadhalika."

Sepp Blatter atazuru baadae Johannesberg na Cape Town kuvikagua viwanja vitatu kati ya vyote 9 vinavyoendelea kujengwa kwa kombe la dunia.Atazuru pia uwanja wa Soweto utakaofungua na kufunga dimba la kombe la dunia.

Katika ziara yake hii, rais wa FIFA anakutana pia na mwenyekiti wa chama-tawala cha ANC Jacob Zuma na hata rais wa zamani mzee Nelson Mandela na FW de Klerk.

Tuklibakia Afrika,huko Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo, mashabiki 13 wa dimba wameuwawa huko Butembo,Kivu ya kaskazini baada ya kuzuka machafuko uwanjani wakati wa mpambano kati ya timu ya SOCOZAKI na NYUKI.Mashabiki wa Nyuki waliituhumu SOCOZAKi kufanya uchawi uwanjani baada yakutiwa bao.Polisi walitumia hewaya kutoa machozi kuwatawanya mashabiki na kiongozi wa polisi alijeruhiwa na yupo hospitalini.

Salehe Mwanamilongo anaripoti kutoka Kinshasa:

Na huko Afrika Mashariki,mashabiki wa Tanzania wanasubiri kwa hamu kuu mpambano wa Septemba 26 kati ya Simba na Young Afficans -mojawapo ya changamoto za Ligi kuu.