1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulio ya kigaidi yaua 91 nchini Norway

Mtullya, Abdu23 Julai 2011

Watu 91 wameuawa katika mashambulio mawili ya kigaidi nchini Norway.Waziri Mkuu wa nchi hiyo,Jens Stoltenberg amesema,si chini ya watu 80 waliuawa kwenye kambi ya vijana pekee, kisiwani Utoya karibu na mji mkuu Oslo.

https://p.dw.com/p/Rbc5
The scene after an explosion in Oslo, Norway, Friday July 22, 2011. A loud explosion shattered windows Friday at the government headquarters in Oslo which includes the prime minister's office, injuring several people. Prime Minister Jens Stoltenberg is safe, government spokeswoman Camilla Ryste told The Associated Press. (AP PHOTO / Holm Morten, Scanpix) NORWAY OUT
Majengo yaliyoteketezwa katika mji mkuu OsloPicha: dapd

Mtu aliejifanya kuwa polisi aliingia katika kisiwa hicho na kufyatua risasi.Polisi wamemkamata mtu mmoja mwenye umri wa miaka 32 kuhusiana na mashambulio hayo. Mawasiliano ya mtandao wa Internet ya mtuhumiwa huyo, yameashiria kuwa yeye ni mtu mwenye itikadi kali za mrengo wa kulia. Hata hivyo, hakuna ishara zinazoonyesha kuwa mtu huyo anahusiana na magaidi wa kimataifa.

Wakati huo huo, serikali za nchi mbalimbali duniani zimelaani mashambulio hayo ya kigaidi. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema kuwa ameshtushwa na mashambulio hayo na kwamba serikali yake na watu wa Ujerumani watasimama pamoja na watu wa Norway.

Umoja wa Ulaya pia umesema umeshtushwa na kile kilichoitwa mashambulio ya kutia uchungu yaliyofanywa katika nchi inayosifika kwa juhudi zake za kuleta amani duniani.

Rais Barack Obama ametoa rambi rambi kwa watu wa Norway. Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, William Hague pia ametoa rambi rambi kwa wahanga na familia za watu waliothirika na mashambulio na amelaani aina zote za ugaidi.