1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya anga ya Israel yaua Wapalestina 4

1 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CVTi

Wapalestina 4 wa kundi la Hamas wameuawa katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Israel katika Ukanda wa Gaza.Kwa mujibu wa maafisa wa Kipalestina watu 9 pia walijeruhiwa katika shambulizi hilo.Jeshi la Israel limethibitisha kuwa liliwashambulia watu hao baada ya kuwagundua karibu na mpaka wake,mashariki ya mji wa Khan Younis.Israel imeimarisha operesheni zake za kijeshi katika Ukanda wa Gaza,tangu Hamas kudhibiti eneo hilo kwa nguvu mwezi wa Juni.