1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya bomu yaua watu 26 Irak

8 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CZ1b

Washambuliaji wawili wa kujitolea maisha muhanga,wameua watu 26 katika mashambulizi mawili mbali mbali nchini Irak.Kwa mujibu wa polisi, watu 16 waliuawa na wengine 30 walijeruhiwa katika mji wa Muqdadiyah,baada ya mshambuliaji mmoja wa kike kuripua mabomu yaliyopachikwa nguoni.Yeye alilenga ofisi ya kundi la Wasunni wanaoshirikiana na vikosi vya Kiiraki na Marekani kupambana na wafuasi wa Al Qaeda.

Katika shambulizi la pili,mwanamgambo aliejitolea maisha muhanga alibamiza gari lake kwenye kituo cha ukaguzi katika mji wa Al-Mansuriyah.Watu 10 waliuawa na 8 walijeruhiwa katika shambulizi hilo.