1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya bomu yaua watu 6 Nigeria

Martin,Prema/dpa17 Juni 2011

Watu 6 wameuawa katika mashambulizi mawili ya bomu siku ya Alkhamisi nchini Nigeria.

https://p.dw.com/p/RU47

Katika shambulizi moja la kujitoa mhanga, bomu liliripuliwa katika gari mbele ya makao makuu ya polisi katika mji mkuu Abuja. Watu 2 waliuawa katika shambulio hilo na lilisababisha magari kadhaa kushika moto.

Saa chache baadae, bomu jingine liliripuka karibu ya kanisa katika mji wa Damboa ulio katika jimbo la Borno kaskazini-mashariki ya Nigeria. Kwa mujibu wa polisi, vijana 4 waliuawa na mtu mmoja alijeruhiwa.

Kundi la madhehebu ya Boko Haram lenye itikadi kali za Kiislamu limedai kuwa ndio lililohusika na shambulio la Abuja.