1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya kigaidi mjini Barcelona ni unyama

Sekione Kitojo
21 Agosti 2017

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo hii wamejishughulisha zaidi na shambulio la kigaidi mjini Barcelona, na mkasa wa  kuondolewa mshauri mkuu wa mikakati wa rais Donald Trump Ikulu ya White House nchini  Marekani.

https://p.dw.com/p/2iYPs
Spanien Las Ramblas in Barcelona
Maombolezo mjini BarcelonaPicha: DW/S. Sezer Bilen

Inaelekea  kukaribia  kufikia  mwisho  kwa  kundi  linalojiita Dola  la  Kiislamu  hatari  ya  mashambulio  ya  kigaidi inaongezeka, kwa  kuwa  wapiganaji  wa  kundi  hilo hataki tena  kurejea  upande  wa  kusini. Inatia  hofu  kwamba mbinyo  dhidi  ya  kundi  la  Waislamu  wenye  itikadi  kali wanapanga  kuwaingiza  washambuliaji  wao  katika mataifa  ya  magharibi, ili kulipiza  kisasi  cha  kushindwa kwao. Jumuiya  ya  kimataifa , licha  ya  mafanikio yaliyopatikana, dhidi  ya  kitisho  cha  kundi  la  Dola  la Kiislamu , inahitaji  pamoja  na  hayo, kujihakikishia ulinzi imara,  pamoja  na  kubakia katika msimamo  wetu wa kidini  na kulinda maadili  yetu  kwa  pamoja. Kwa  kuwa mapambano  dhidi  ya  ugaidi  unaohusishwa  na Mwenyezi  Mungu , utaweza  kushindwa  tu  kwa  kutumia nguvu  za  dola  na  sio  kwa kutumia  hali ya  maridhiano yasiyo  sahihi.

Gazeti  la  Lausitzer Rundschau  kutoka  mjini  Cottbus likizungumzia  kuhusu  shambulio  la  kigaidi  nchini Uhispania , linaandika.

Jibu litakalokuwa mjarabu  kabisa  kwa  tukio  kama  hilo la Uhispania , kutokana  na  mauaji  hayo  ya  kuchukiza na wendawazimu waliohusika  katika  mauaji  hayo, ni  pale mtu atakapojizuwia  kubadili  maisha  yake  ya  msingi, licha  ya  ugaidi  huo. Washambuliaji  kwa  upande  wao wanaonesha  chuki  tu  na  matumizi  ya  kinyama  ya nguvu, zaidi  ya  hayo  hakuna. Ilikuwa  jambo  zuri, kwamba wagombea  katika  uchaguzi  siku  ya  Ijumaa walipounguza  shughuli   zao  na  kutoa  ishara  ya  umoja. Tukio  la  kigaidi  pamoja  na maombolezi  ya  wahanga havikutumika , kwa  ajili  ya  kujipatia  umaarufu usiostahili katika  uchaguzi  wa  Ujerumani. Hali  hii inaonesha ukomavu  wa  demokrasia. Sio  kwamba , katika mapambano  ya  kuwania  madaraka  katika  uchaguzi , suala  la  ulinzi zaidi lisizungumziwe,  la  , ni  kunyume chake.

Kwa upande  wa  kuondolewa  kwa  mshauri  mkuu  wa mikakati  kwa  rais  Donald Trump  wa  Marekani  katika Ikulu  ya  Marekani  ya  White House Stephen Bannon , gazeti  la  Fränkischer  Tag la  mjini  Bamberg  linaandika.

Kwa  rais  kutotaja  kwa  jina lake  sahihi  wanazi mamboleo , na  kuanza  kujificha  katika  uongo,  kila  kitu  hapa kinaonekana  kuwamo  katika  mikono  ya  Bannon. Akiwa ni mwenye  msimamo  mkali na  anayetoka  katika  jarida  la habari  la  msimamo  mkali  wa  mrengo  wa  kulia  la Breitbart, sumu  ya Bannon  ataisambazwa  zaidi  hapo baadaye  kwa  kiwango  kikubwa. Pamoja  na  kudhibitiwa kutoka  Ikulu  ya  Marekani  ya  White  House , lakini hakuna mtu mwingine anayeweza  kushindana  nae.

Gazeti  la  Südwest-Presse  la  mjini  Ulm  linazungumzia kuhusu  mjadala  unaoendelea  nchini  Ujerumani kuhusiana  na  kuweka  ukomo  wa  kuruhusu wakimbizi kuingia  nchini  humo. Gazeti  linaandika.

Isisahaulike  kwamba , bila  ya  kuwekwa  ukomo  wa kuruhusu  wakimbizi  kuingia  nchini  humu, hakutakuwa na  makubaliano  ya  muungano  wa  kuunda  serikali. Kusahau  litakuwa  pigo  kwa  kansela  katika  mkutano mkuu  wa  chama  ndugu na  chama  cha  kansela  cha CSU. Hali  ilivyo  sasa  ni  kwamba  ukomo  huo umekwisha  fikiwa.  Je mzigo  huo  sasa  umewekwa  kando ? Ni  kawaida  ya  vyama  hivyo  ndungu , kwamba  katika wakati  wa  kampeni ushindi uwe umehakikishwa  kwa kuondoa  kila  kinachoweza  kuzuwia , ikiwa  ni  pamoja  na mizozo,  kinyume  na  upande  wa  chama  kikuu  cha upinzani  cha  SPD , hali  hiyo haraka imefichwa  chini  ya zulia. Njia  hiyo  haiondoi  uchafu. katika  majadiliano  ya kuunda  muungano  wa  serikali  suala  la  ukomo litajitokeza  bila  shaka.

Msimu  mpya  wa  ligi  ya  Ujerumani  Bundesliga, umeanza rasmi , linaandika  gazeti  la  Badische Neueste Nachrichten  la  mjini  Karlsruhe. Mhariri  anaandika.

Mpira  katika  Bundesliga  umeanza kudunda  tena, na  hii ni  katika  msimu  wa  55. Mafanikio  ya  kandanda  la Ujerumani  tayari  yanaangaliwa  tena. Kuanzishwa  kwa ushahidi  wa  kutumia  vidio  una  maana  ya uamuzi  wa haraka  katika  historia  ya  ligi  hiyo, kuweza  kujua  iwapo kila  kitu  kinakwenda  sahihi , ama  la.

 

Mwandishi: Sekione  Kitojo / inlandspresse

Mhariri: Mohammed Abdul Rahman