1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashariki ya Kati

Ramadhan Ali26 Julai 2007

Rais Bush wa Marekani alenga kuleta ufumbuzi wa mgogoro wa Israel na Palestina kabla kun'gatuka.

https://p.dw.com/p/CHAU
Mawaziri wa nje wa Jordan na Misri ziarani Jeruselem
Mawaziri wa nje wa Jordan na Misri ziarani JeruselemPicha: AP

Rais Mahmud Abbas wa Palestina, amearifui leo kuwa rais George Bush wa Marekani, anasaka suluhisho la mwisho la mgogoro kati ya Israel na Palestina kabla hakuondoka madarakani.

Taarifa hii imeibuka baada ya jana ujumbe unaosemekana wa Jumuiya ya nchi za kiarabu-Arab League kwenda Jeruselem kuutembeza ule mpango wa nchi za kiarabu wa kufikia amani na Israel ikiwa nayo itan’gatuka kutoka ardhi za waarabu.

“Wamarekani wametia nia kuzihimiza pande zinazohusika kufikia mapatano katika kipindi cha sasa cha urais wa George Bush.”-alinukuliwa Mahmud Abbas katika mazungumzo yaliochapishwa hii leo.

Abbas akaongeza, “Nimesikia hayo kwa masikio yangu kutoka kwa rais mwenyewe n a hata kutoka kwa waziri wa nje Dr.Condoleeza Rice.Wanataka kufikia muafaka baina ya waisrael na wapalestina mnamo mwaka ujao.”

Rais George Bush anaacha madaraka hapo januari,2009 baada ya kupitisha awamu 2 katika Ikulu.

Rais Mahmud Abbas amesema liundwe dola la wapalestina ndani ya ile mipaka ya 1967 huku sehemu ya mashariki mwa Jeruselem iwe mji mkuu wake pamoja na ufumbuzi wa matatatizo yote yaliopo miongoni mwayo lile la wakimbizi .

Akiulizwa iwapo ana nia ya kugombea uchaguzi ujao wa rais ,hakusema ndio au la.”labda miaka 3 na nusu yatosha.” Aliliambia gazeti la Maarif la Israel.Maariv limedai kuwa Abbas amemungamkono Marwan Barghuti,mfungwa mashuhuri wa kipalestina aliomo korokoroni nchini Israel.

Gazeti la Haaretz la Israel, limeripoti nalo kuwa waziri mkuu Olmert, amejitolea kufanya mazungumzo kuafikiana kanuni za kimsingi za kuunda dola la kipalestina likiwa na Jeruselem mji mkuu wake hata kabla maswali nyeti zaidi ya kidiplomasia kuguswa.

Ujumbe wa Jumuiya ya nchi za kiarabu-Arab League ingawa uliingiza mawaziri wa nje wa Misri na Jordan,ulikuwapo jana Jeruselem kuutembeza mpango wa waarabu wa kubadilishana yamani kwa ardhi.Ulionana na waziri mkuu Olmert na rais pamoja na kutembelea bunge la Israel-KNESET.

Wakati viongozi hao wa Israel na wa kiarabu walilahkiana kwa dhati,pande zote mbili ziliungama kwamba, mashauri ya Arab League, hayawezi kukika, mazungumzo ya moja kwa moja baina ya Israel na wapalestina.

“Mashauri haya muwafaka, yanatoa fursa ya kipekee na kihistoria kufikiwa mapatano.” –alisema Abdul-Ilah Khatib,waziri wa nje wa Jordan wakati wa mkutano na waandishi habari huku waziri wa nje wa Israel Tzipi Livni, na yule wa Misri Aboul Gheit, wakiwa ubavuni mwake.Akaongeza, mashauri hayo yataipa Israel usalama,kutambuliwa na kukubaliwa katika eneo hilo-jambo ambalo daima likitakiwa na Israel.