1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashariki ya Kati

11 Mei 2007

Waziri wa nje wa Israel Livni akutana Cairo na mawaziri wa nje wa Misri na Jordan kuzungumzia mpango wa amani wa nchi za kiarabu.Mpango huo unalenga kubadilishana amani kwa ardhi.

https://p.dw.com/p/CHET

Israel na waakilishi wa dola za kiarabu wamekutana jana kwa mara ya kwanza mjini Cairo, kuzungumzia mashauri yaliotolewa na nchi za kiarabu juu ya ufumbuzi wa mzozo wa Mashariki ya kati.Waziri wa nje wa Israel, Zipi Livni, aliueleza mkutano wake na mawaziri wa nje wa Misri Ahmed Abul Gheit na wa Jordan Abdul Khatib ni wa kihistoria.

Jumuiya ya nchi za kiarabu-Arab League imelezea utayarifu wake kwa mara ya kwanza tangu kupita nusu karne kupeleka ujumbe wake Israel kwa mazungumzo.Kueleza mkutano huo kuwa ni wa kihistoria kama alivyosema livni ni haraka mno. Juu ya hivyo, mkutano huo na mawaziri wa Misri na Jordan zaidi ungetia tamaa ya kuutatua mzozo kati ya Israel na warabu laiti hali ya ndani tangu nchini Israel hata katika ardhi za wapalestina ingelikuwa nzuri wakati huu.

Kwani, masharti ya amani tangu katika eneo la Mashariki ya Kati hata ulimwenguni ni bora kuliko yalivyokuwa muda mrefu kabla.Changamoto inayotolewa na Iran –dola lenye kupata nguvu katika Ghuba-zinazifanya dola nyingi za kiarabu za waumini wa madhehebu ya sunni kuingiwa na wasi wasi na wsahka .

Syria na rais wake mchanga Bashar al-Assad ingeweza, kwa kuikomboa milima yake ya Golan,kuimarisha utawala wake.Na Ujerumani ikiwa sasa mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya ,imekwishafanikiwa kwa kuyafufua mazungumzo ya pande 4-juu ya mashariki ya kati-UU,Russia,UM na Marekani.

Na kwa mpango wa amani uliotungwa na Saudi Arabia 2002, kubadilishana amani kwa ardhi-kuna msingi barabara wa majadiliano.Bila shaka ,Israel haitaukubali mpango huo kikamilifu.Lakini, ni mpango umbao unanyemelea matakwa ya jamii ya kimataifa na unauweka mgogoro wa Israel na wapalestina juu ya msingi wa suluhisho la dola 2 bega kwa bega na kutambuliwa kwa Israel na dola za kiarabu.

Waziri wa nje wa Israel Livni ameipongeza juhudi hii huko Cairo zaidi kuliko alivyofanya waziri mkuu Ehud Olmert. Hakuna ajuwae kwa muda gani waziri mkuu Olmert anaekabiliwa na msukosuko wa ndani atadumu madarakani na nini hali ya siku za usoni za waziri huyu wa nje Livni.

Hata upande wa wapalestina, kuna wasi wasi na hali ya kuregarega:Serikali ya umoja wa taifa kati ya Fatah –chama kinachoelemea magharibi na Hamas cha kiislamu ,haifanyi kazi bila ya mvutano.

Kama nchini Israel, uchaguzi mpya hata upande wa wapalestina wamkinika.Rais wa Mamlaka ya ndani ya wapalestina,Mahmoud Abbas ingawa yutayari kufikia mapatano na Israel,lakini mamlaka yake si makubwa hivyo.

Isitoshe,matumizi ya nguvu yanaendelea kutokea pande zote mbili,pia azma za Israel kuendelea kujenga maskani za wayahodi katika mashariki mwa Jeruselem,hakusaidii kufumbua kitandawili hiki.

Maarifa lakini, yanatufunza kuwa mapatano ya amani katika Mashariki ya kati, yaweza tu kufikiwa na wanasiasa wanaokubalika nchini –wanasiasa wa aina hiyo wenye nguvu tangu upande wa Israel hata wa Palestina, ni bidha ilio adimu wakati huu.