1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashariki ya Kati

6 Agosti 2008

Olmert akutana na Abbas na Assad wa syria na Erdogan wa uturuki.

https://p.dw.com/p/ErYN

Wakati makamo wake Shaul Mofaz,mzaliwa wa Iran anaeitishia Iran vita ameanza kampeni ya kugombea cheo chake , waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert anakutana na Rais wa Mamlaka ya Ndani ya wapalestina Mahmud Abbas mjini Jeruselem-wiki baada ya Bw.Olmert kutangaza azma ya kujiuzulu.

Rais Bashir Al Assad wa Syria nae amekuwa na mazungumzo na waziri mkuu wa Uturuki Tayyip Erdogan huko Uturuki juu ya amani ya Mashariki ya kati .

►◄

Ziara ya Rais Bashir Al- Assad wa Syria katika kituo cha kitalii cha Bodrum nchini Uturuki,katika mwambao wa pwani wa Aegean imefanyika wiki tu tangu

Israel na syria kumaliza duru ya 4 ya mazungumzo yao chini ya usimamizi wa uturuki mjini Istanbul bila kufaulu kuanzisha mazungumzo ya uso kwa uso kati yao.

duru ijayo ya mazungumzo yasio ya moja kwa moja baina ya syria na israel yatazamiwa kuwa kati ya mwezi huu.Uturuki inahofia kuwa msukosuko wa ndani nchini Israel ambako waziri-mkuu Olmert anapanga kujiuzulu karibuni, kutazidi kutatanisha mambo na kuzuwia pande hizo mbili kukutana uso kwa uso.

Taarifa zilizotolewa hadharan zinaonesha pia Syria na Israel zingali zimegawika juu ya maswali ya kimsingi mfano kukalia Israel kwa milima ya golan na usuhuba iliofunga syria na jirani yake Iran,Hizbollah nchini Lebanon na chama cha Hamas cha wapalestina.

Waziri mkuu wa uturuki erdogan alimkaribisha rais assad na mkewe katika uwanja wa ndege wa Bodrum kabla hawakwenda katika hoteli moja ya kifahari kwa chakula cha mchana kabla mazungumzo yao ya faragha.

Rais Assad na waziri mkuu Erdogan wamekutana mara kwa mara na wanafahamika kuwa na usuhuba mzuri.

Gazeti maarufu la Uturuki-Hurriyet limearifu kwamba mradi wa kinuklia wa Iran pia ulikua mada ya mazungumzo yao.

Na mjini Jeruselem, waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert anakutana leo na rais Mahmud abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Wapalestina-wiki baada ya Bw.Olmet kuelezea nia yake ya kujiuzulu na kuutia matatani utaratibu wa amani unaosimamiwa na Marekani.

Makamo wa waziri mkuu na waziri wa zamani wa mambo ya ulinzi mwenye siasa kali mzaliwa wa Iran, Shaul Mofaz ameanza kampeni yake ya kugombea cheo cha Bw.Olmert.

Akiwa na umri wa miaka 59,amedai vita na nchi aliyozaliwa Iran, yamkini haviepukiki kutokana na mradi wa Iran wa kinuklia.Mofaz alipata sifa na umashuhuri alipotumia mkono wa chuma kukandamiza uasi wa wapalestina 2000 tangu akiwa mkuu wa majeshi na baadae waziri wa ulinzi.

Akiwa sasa ni waziri wa usafiri ni mmmoja kati ya viongozi 2 wa usoni kabisa katika chama cha Kadima wanaogombea wadhifa huo.Mwengine ni waziri wa nje Bibi Tzipi Livni.