1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashauriano ya kuunda serikali mpya yaendelea

9 Februari 2008

Waziri mkuu mpya kuapishwa leo

https://p.dw.com/p/D4p7

DARESAALAM

Mashauriano ya kuunda serikali mpya yanaendelea nchini Tanzania baada ya hapo jana rais Jakaya mrisho Kikwete kumteua waziri mkuu mpya bwana Mizengo Peter Pinda kufuatia kujiuzulu kwa waziri mkuu wa zamani Edward Lowasa anayekabiliwa na tuhuma za kuhusika na kashfa nzito ya rushwa inayohusu kandarasi ya nishati na kampuni moja ya Marekani.Waziri mkuu mpya bwana Pinda ambaye alikuwa ni waziri wa nchi tawala za mikoa na serikali za mitaa ataapishwa hii leo baada ya kuidhinishwa na bunge hapo jana mjini Dodoma.

Taarifa zinasema baraza jipya la mawaziri huenda likatangazwa jumatatu ijayo.Kwa mujibu wa uchunguzi kuhusu mkataba wa Nishati bwana Lowassa pamoja na mawaziri kadhaa wa serikali na maafisa wengi wengine wanadaiwa walihusika katika tenda ya kuipendelea kampuni ya Richmond iliyo na makao yake mjini Texas Marekani.Kashfa hiyo pamoja na kujiuzulu kwa waziri mkuu mapema wiki hii kulisababisha mshtuko mkubwa katika taifa hilo ambalo limekuwa katika miaka ya hivi karibuni likibeba sifa nzuri katika jumuiya ya wafadhili wa kimataifa.