1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashindano ya kuania kiti cha rais wa Marekani

Lausch, Walter 6 Machi 2008

Kishindo kwa chama cha Democrats kinazidi wakati warepublican wameshamchagua mgombea wao

https://p.dw.com/p/DJLt
Hillary Clinton mgombea mmojawapo wa chama cha DemocratsPicha: AP

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo wamemulika kwa mapana na marefu mashindano ya kuania tikiti ya vyama vya Republican na Democrats  kugombea wadhifa wa rais uchaguzi utakapoitishwa Marekani November mwaka huu.Wahariri wengi wanahisi kwa upande wa chama cha Democrats kinyang'anyiro kati ya wagombea wawili kinazidi kusisimua.Senator Hillary Clinton amezuwia ushindi mfululizo wa mpinzani wake chamani Barak Obama alipoibuka na ushindi Texas,Ohio na Rhode Island.Gazeti la DRESDNER NEUESTEN NACHRICHTEN linachambua:


"Anastahiki kuvuliwa kofia:Bibi huyo shupavu,senetor wa New-York amedhihirisha anaweza.Mageuzi yanayopigiwa upatu na Obama hayajawababaisha watu jumanne hii.Mambo yamebakia kama yalivyokua Clinton anashinda katika miji mikubwa na Obama miji midogo.Obama kamtia munda Clinton lakini hakumuangusha.


"Wote waliofikiria Hillary Clinton yake yamekwisha,amejidanganya.Na kusema kweli lingekua kosa kuamini kwamba senetor huyo wa New-York kweli kapigwa kumbo.Ikulu ya Marekani ni ukumbi wake Hillary Clinton,na sio kama mke wa rais,bali kama rais hasa.

Kwa maoni ya STUTTGARTER ZEITUNG mashindano ya wagombea hao wawili yanaweza kuwa na hatari kwa chama cha Democrats.Gazeti linaendelea kuandika:


"Wagombea hawa wawili wanaijongela njia ya sirata.Hakuna ajuaye kama wataweza kudhibiti mkondo wa hujuma wanazotupiana.Hasimu yao wa  chama cha Republican John McCain ameshajikwamua . Kuna mada kadhaa zinazohitaji kushughulikiwa kuanzia Irak hadi kufikia sera za kiuchumi.McCain anawakati wa kutosha hivi sasa kuzungumzia mada hizo.Na kusema kweli yeye ndie mshindi wa kweli wa mashindano ya jumanne iliyopita -ameshajikingia sauti za wajumbe wote wanaohitajika ili aweze kuteuliwa kugombea wadhifa wa rais wa Marekani."


Maoni sawa na hayo yametolewa pia na mhariri wa gazeti la DIE TAGESZEITUNG anaeandika:


"March nne mwaka 2008 ni tarehe inayoweza kuingia katika madaftari ya historia ya Marekani,kama siku iliyoshuhudia kuchaguliwa John McCain kua rais wa 44 wa Marekani.Katika wakati ambapo McCain amejipatia thibitisho timamu  la kuwa amgombea wa chama cha Republican,wademocrats wameitupa fursa ya mwisho ya kumteuwa mtu anaeweza kupigania nafasi ya kuingia ikulu ya Marekani bila ya kutanguliza mbele hujuma.Hillary Clinton amethibitisha ushindi wake katika miji mitatu,ni matokeo ya hujuma zake dhidi ya Barack Obama.Kwa hivyo ataendelea na mkondo huo huo.Lakini kwa kuendelea kumhujumu Obama,anachanagia pia kuwafanya wapiga kura wakike na wakiume ambao hawampendi,wazidi kumchukia.Na wakati huo huo anafanya kazi ambayo kimsingi iliokua ya John McCain na chama chake cha Republican.


Gazeti la FRANKFURTER RUNDSCHAU linazungumzia pendekezo la bibi Clinton la kutaka kushirikiana na Obama.Gazeti linaendelea kuandika:


"Sio tuu kwa wagombea,shinikizo linawakaba pia wapiga kura kutaka iamuliwe haraka.Wengi wa wafuasi wa chama cha Democrats wanataka kuona ushirika naiwe kati ya Clinton na Obama au Obama na Clinton.Linapohusika suala la madaraka nchini Marekani anaejulikana ni mshindi na aliyeshindwa tuu.Hakuna atakaeridhika na cheo cha makamo wa rais kwa wakati wote ule ambao nafasi ya kuingia ikulu ya white House ipo,hata kama Hillary Clinton ameshagusia uwezekano huo.Kwa hivyo mapambano yanaendelea.Hakuna lakini Mdemocrats yeyote anaetaka kuona chama chao kikila hasara kwa kuibuka wagombea wawili wa kihistoria-mmarekani mweusi au mmarekani wa jinsia ya kike.