1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashindano ya riadha Osaka kuanza leo

Ramadhan Ali23 Agosti 2007

Mashindano ya 11 ya riadha ulimwenguni yanaanza mjini Osaka, Japan na yataendelea hadi Septemba 2.Wanariadha wa afrika mashariki na hasa Ethiopia na Kenya tangu wakike hata wa kiume ,wanatarajiwa kutamba katika masafa ya kati na marefu-miongoni mwao ni T.Dibaba.

https://p.dw.com/p/CHbB
Hutaweza kushinda hivyo Osaka!
Hutaweza kushinda hivyo Osaka!Picha: AP

Wasichana 3 wa Ulaya na mmoja wa kiafrika, wanatazamiwa kuandika historia katika mashindano ya riadha ya ubingwa wa dunia yanayoanza leo mjini Osaka,Japan:Nao ni mrusi anaeruka kwa upongoo (Pole Vault)- Yelena Isinbayeva,bingwa wa dunia wa michezo 7 “heptathlete” Carolina Kluft, kutoka Sweden,mrukaji high jump,Blanka Vlasic wa Croatia na muethiopia Tirunesh Dibaba,mwanamke wa kwanza kushinda mbio za mita 5000 na 10.000 kwa pamoja huko Helsinki,miaka 2 iliopita.

Muethiopia Dibaba mara hii aweza kutolewa jasho kali zaidi miongoni mwa wanariadha hao 4 wa kike:Yeye atajaribu tena mjini Osaka, kushinda mbio za mita 5000 na 10.000 .

Akishinda mita 5000 atakuwa msichana wa kwanza kushinda masafa hayo katika mashindano 3 .Ushindi wake kjatika mita 10.000 pia utakuwa wa kuvutia,kwani hakuna msichana aliewahi kutetea taji lake la dunia katika mbio hizo.

Upinzani mkali utatoka kwa mwenzake wa Ethiopia, Meseret Defar na pia katika mita 10.000 changamoto itatoka pia Ethiopia kwa dada mkuu Ejegayehu Dibaba na Meseret Tufa.Kwahivyo, ni waethiopia weenyewe kwa wenyewe,ikiwa wasichana wa Kenya, watanisamehe hapo,waweza kutiliana vitumbua vya mchanga.

Kama Dibaba,nafasi zao za kurejea ushindi wao zitategemea na hali ya joto kali la Osaka.Mrusi Isinbayeva anawsasi wasi joto hilo laweza likaathiri uruikaji wake kwa upongoo.Azma yake kuu lakini huko Osaka, asema ni kushinda tu na sio kuweka rekodi kama katika mashindano yaliopita.

Kwani, rekodi amepachika za kutosha-jumla ya 20 tena za dunia pamoja na 11 za mashindano ya ukumbini-indoors.Kluft wa Sweden,anatumai kuwa msichana wa kwanza kushinda mataji 3 ya mashinda no7 mbali mbali-hetathlon.Akiwa hajashindwa tangu 2001,mswede amekuwa mwanariadha wa kwanza kuteta ushindi wake wa 2003 na 2005.

Mcroatia Vlasic, atalenga shabaha yake kuweka rekodi ya dunia katika High jump.Msichana huyu wa miaka 23 amesharuka mita 2.07cm msimu huu akikaribia kuifikia rekodi ya Mbulgaria Stefka Kostandinova ya mita 2.09.Aliiweka katika mashindano ya 1987.

Bingwa mara 2 wa mbio za mita 1.500 mrusi Tatyana Tomashova,hatahudhuria mashindanmo ya Osaka kwavile ameumia mguu.Lakini, mrusi mwenzake Yelena Saboleva ndie anaeongoza duniani wakati huu.Mshindi wa mbio za kasi za mita 100 wa Helsinki Allyson Felix, kutoka Marekani, anapigiwa upatu kutamba masafa ya mita 100,malkia ni bingwa wa Marekani Lauryn Williams.

Yeye atapewa changamoto na mjamiaca bingwa wa olimpik Veronica Campbell na bingwa wa 2003 wa dunia Torri Edwards wa Marekani.

Bingwa mtetezi katika masafa ya mita 400 kuruka viunzi,Yuliya Pechonkina wa urusi,anarudi uwanjani kutetea taji lake lakini anakabiliwa na changamoto kali kutoka kwa bingwa wa 2003 Jana Rawlinson wa Australia.

Msichana wa Ujerumani, Franka Dietzsch, anatapia taji lake la 3 katika kurusha kisahani –Discuss.Alishinda 1999 na 2005.Mjerumani mwenzake Christina Obergfoll, anaongoza duniani katika kurusha mkuki-javelin.Tusubiri basi bunduki kulia leo mjini Osaka,Japan.