1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Masoko ya hisa duniani yazidi kuporomoka

22 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cw6j

NEW YORK:

Masoko ya hisa katika mataifa mengi ya Ulaya yameporomoka mapema leo kutokana na kuendelea kudorora kwa uchumi wa Marekani ambao baado unazifanya roho za wawekezaji kuwa na wasiwasi.

Katika soko la Ujerumani la hisa la DAX bei ya hisa ilikuwa chini kwa asili mia 2 baada ya hasara ya zaidi ya asili mia 7 jana jumatatu-ambayo hii ndio hali mbaya kuwahi kutokea tangu mwaka wa 2001.Wafanya biashara wa Ulaya baado wanawasiwasi wakisubiri kuona hali itakuwaje katika soko la hisa la New York Marekani ambalo limefunguliwa baada ya kufungwa jana kwa ajili ya siku kuu.

Hali hiyo imeleta wasiwasi katika sekta ya fedha duniani.