1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Masuali yaulizwa kuhusu mshukiwa wa mauaji Ufaransa

23 Machi 2012

Maafisa nchini Ufaransa wanakabiliwa na maswali jinsi mshukiwa mwenye itikadi kali za kiislamu ambaye alikuwa amejulikana, alivyoweza kuwauwa watu saba, katika mashambulizi matatu tofauti kabla ya kuuliwa na polisi.

https://p.dw.com/p/14Phn
Masked French special unit policemen (RAID) arrive at Perignon barracks after the assault to capture gunman Mohamed Merah during a raid on a five-storey building to arrest a suspect in the killings of three children and a rabbi on Monday at a Jewish school, in Toulouse March 22, 2012. The 23-year-old gunman suspected of killing seven people in southwestern France in the name of al Qaeda, jumped from a window to his death in a hail of bullets after police stormed his apartment on Thursday. France's Interior Minister said earlier police hoped to capture Mohamed Merah, who had confessed to police negotiators to killing three soldiers as well as three Jewish children and a rabbi at a school, alive. REUTERS/Pascal Parrot (FRANCE - Tags: CRIME LAW CIVIL UNREST)
Frankreich Terror Mohamed Merah Toulouse RAID AbzugPicha: Reuters

Kwa kuwaongezea shinikizo maafisa wa usalama, afisa mmoja wa polisi mkongwe ameuliza jinsi mshukiwa huyo hakuweza kukamatwa akiwa hai wakati wa uvamizi wa jana Alhamisi katika mji wa Kusini Magharibi wa Toulouse. Polisi kutoka kitengo maalum waliingia ndani ya jengo hilo baada ya kulizingira kwa zaidi ya saa 32, na kumuuwa mtu huyo kwa jina la Mohamed Merah aliyedai kuwa ni mwanamgambo wa kundi la al-Qaeda, alipojaribu kufyatua risasi kiholea akitoroka kutoka chumbani mwake.

Tukio hilo lilikuwa limekatiza shughuli za kampeni za uchaguzi wa rais nchini Ufaransa uliopangwa kufanyika Aprili na Mei, lakini Sarkozy alirejelea kampeni yake akitaka kuchaguliwa tena, kwa kuhutubia mkutano wa hadhara mjini Strasbourg jana jioni, ambapo alisema uhalifu huo haukuwa kazi ya mtu mwenye akili punguani. Alisema uhalifu huo ulikuwa ni kazi ya mtu mwenye tabia ya kinyama.

Awali katika taarifa yake iliyorushwa kupitia televisheni, Sarkozy aliapa kuwasaka watu wenye itikadi kali, akisema atawachukulia hatua za kisheria watu wanaozitembelea tovuti za kigaidi au kusafiri hadi mataifa ya ng'ambo kupokea mafunzo ya imani za aina hiyo.

Masked French special unit policemen (RAID) arrive at Perignon barracks after the assault to capture gunman Mohamed Merah during a raid on a five-storey building to arrest a suspect in the killings of three children and a rabbi on Monday at a Jewish school, in Toulouse March 22, 2012. The 23-year-old gunman suspected of killing seven people in southwestern France in the name of al Qaeda, jumped from a window to his death in a hail of bullets after police stormed his apartment on Thursday. France's Interior Minister said earlier police hoped to capture Mohamed Merah, who had confessed to police negotiators to killing three soldiers as well as three Jewish children and a rabbi at a school, alive. REUTERS/Pascal Parrot (FRANCE - Tags: CRIME LAW CIVIL UNREST)
Frankreich Terror Mohamed Merah Toulouse RAID AbzugPicha: Reuters

Kampeni za uchaguzi wa rais kuendelea

Kinyang'anyiro cha uchaguzi wa rais kinarejea leo, na masuala yatakayoangaziwa sasa ni ugaidi, usalama, na mtazamo wa itikadi kali nchini humo. Rais Sarkozy atazuru mji wa Kaskazini Valenciennes ambapo anatarajiwa kuikagua miradi ya ukarabati, viwanda, na vyumba vilivyojengwa kwa ajili ya wafanyakazi.

Wanasiasia kadhaa wanauliza jinsi maafisa wa ujasusi wa Ufaransa walishindwa kukomesha msururu wa mauaji yaliyofanywa na Merah ikizingatiwa kuwa alikuwa kwenye orodha ya watu wenye itikadi kali. Mpinzani mkuu wa Sarkozy, Francois Hollande, alisema maswali ni lazima yaulizwe. Kura ya maoni imemwonyesha Sarkozy akiwa mbele ya mpinzani wake Hollande katika duru ya kwanza ya uchaguzi Aprili 22, ijapokuwa ilitabiri Hollande kushinda katika duru ya pili ya Mei 6. Wapiga kura wamemwona Sarkozy kuwa mkweli kuhusu masuala ya usalama na uhamiaji ambayo yanazungumziwa zaidi katika kampeni.

Mshukiwa alikuwa kwenye orodha ya Marekani

Kiongozi mmoja wa ujasusi nchini Marekani alisema mshukiwa huyo alikuwa kwenye orodha ya watu waliopigwa marufuku kusafiri kwa ndege. Orodha hiyo iliundwa na maafisa wa Marekani, inawapiga marufuku wale waliotajwa kusafiri kwa ndege hadi na kutoka nchini humo.

Rais Sarkozy ametaka kuwepo utulivu wakati uchunguzi wa mauaji ukiendelea
Rais Sarkozy ametaka kuwepo utulivu wakati uchunguzi wa mauaji ukiendeleaPicha: Reuters

Wakati huo huo Waislamu nchini Ufaransa wanahofia kutengwa kutokana na tukio hilo. Kiongozi wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Front National Party Marine le Pen alikuwa miongoni mwa wale wa kwanza kushutumu itikadi kali za Kiislamu akidai kuwa kila mara amekuwa akionya kuhusu athari zake.

Akizungumza wakati wa kampeni yake jana Le Pen alisema kwa miaka kumi sasa amekuwa akionya kuwa athari ya itikadi kali za kiislamu haitiliwi maanani nchini Ufaransa.

Mwandishi: Bruce Amani/Reuters/AFP/IPS

Mhariri: Josephat Charo