1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa ya Afrika yaahidi kusalia ICC

1 Novemba 2016

Nchi nyingi zimetangaza kuendelea kuiunga mkono mahakama ya Kimataifa inayoshughulikia kesi za jinai ICC, katika mkutano wa nchi 193 wanachama wa ICC wiki kadhaa baada ya nchi tatu za bara la Afrika kutangaza kujitoa.

https://p.dw.com/p/2RyaH
GMF Logo Interantional Crime Court ICC

Kauli ya mataifa kuendelea kuiunga mkono mahakama hiyo imetolewa jumatatu hii (31.10.2016) huku mengi kati ya mataifa hayo yakitaka kuwepo kwa mazungumzo kati ya ICC na Umoja wa Afrika katika matumaini ya kuangazia wasiwasi wa bara hilo na  pia kuangalia upya uamuzi wa Burundi, Afrika kusini na Gambia wa kutaka kujitoa ICC.

Balozi wa Kenya katika mahakama hiyo ya Kimataifa Tom Amolo hajaweka wazi  msimamo wa nchi yake,kuwa itataka pia kujitoa ama la japo aliwambia wanachama 193 wa chombo hicho  kuwa nchi yake imekuwa  ikifuatilizia kwa makini madai ya mataifa mengine kujitoa.

Balozi wa Tanzania katika umoja  wa mataifa Tuvako Manongi alisema kuwa mahakama hiyo inauhusiano unaoyumba na Afrika hali ambayo imezua hofu kwa mataifa hayo kuanza kujitoa.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-Moon,kwa upande wake amesema dunia inahitaji kujenga mfumo wa upatikanaji haki kwa kupitia mahakama hiyo

"ICC na mahakama nyingine  vimetengeneza mfumo wa kutoa haki kwa watu wanaofanya makosa , pamoja na kuwa tunafahamu kuwa kumekuwa na madhaifu, mashitaka yanaweza kuchukua muda mrefu kuliko matarajio, sio kila nchi inatarajia ICC kutoa maamuzi pamoja na kuwa nchi nyingine zinategemea lakini wamekuwa hawaisaidii ICC" alisema Ban

UN-Generalsekretär Ban Ki-moon
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moonPicha: Picture-Alliance/M. Girardin/Keystone

Nigeria, nchi ambayo ina watu wengi  zaidi barani afrika pamoja na Senegal ambayo imekuwa nchi ya kwanza kuridhia  mkataba wa Rome ambao ulianzisha mahakama hiyo na Tanzania wamesema kuwa bado wanaendelea kuiunga mkono mahakama ya ICC  huku wakielezea umuhimu wake katika kupambana na   makosa ya mauaji ya kikatili  ambayo yamekuwa yakifanyika duniani, hii ikiwa inajumuisha mauaji ya kimbari.

Mahakama ya ICC inashutumiwa na baadhi ya viongozi wa afrika kuwa imekuwa ikifanya upendeleo kwa sababu tangu mkataba wa Rome uanze kufanya kazi mwaka 2002, ni watu wanne tu ambao wamepatikana na hatia ya kuhusika na uhalifu wa kibinadamu na uhalifu wa kivita watatu wakiwa ni kutokea nchini Congo na mmoja kutoka nchini Mali.

Inaonyesha kuwa inawalenga washutumiwa kutoka Bara la Afrika, na katika idadi ya uchunguzi wa visa 10 unaendelea hivi sasa, visa 9 ni kutoka Afrika na kisa kimoja ni kutoka kwingineko iliyokuwa jamhuri ya kisoviet ya Geogia, ICC kwa upande wake imekuwa ikiongeza ufanyaji kazi wake duniani, kwa sasa inafanya uchunguzi wa awali wa makosa  ili kuweza kuona kama inaweza kufungua uchunguzi uliokamilika katika mataifa ya Afghanistan, Ukraine, and Colombia pamoja na mipaka ya palestina na shutuma za makosa kwa majeshi yaUingereza nchini Iraq

Akiwasilisha ripoti ya mwaka rais wa ICC hakimu Silvia Fernandes de  Gurmendi alisema kuwa kesi mbili zinaendelea na moja imepangwa kuanza kusikilizwa hivi karibuni,kufuatika kupatikana na hatia kuna utaratibu wa fidia kwa waathirika pia katika kesi nne.

Mwandishi: Celina Mwakabwale/AP

Mhariri:Yusuf Saumu