1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Mataifa ya Kiarabu yaikubali Syria baada ya miaka 11

Sudi Mnette
8 Mei 2023

Umoja wa nchi za kiarabu umeikaribisha Syria katika umoja huo, na kuhitimisha kusimamishwa kwake kwa zaidi ya muongo mmoja na kuhakikisha pia Rais Bashar al-Assad anarejea katika kundi lao.

https://p.dw.com/p/4R1Ly
Ägypten I Treffen der Arabischen Liga in Kairo
Picha: Khaled Desouki/AFP

Taarifa ya uamuzi huo inasema Syria inaweza kuanza tena ushiriki wake Mikutano ya Umoja wa Kiarabu mara moja, huku ikitoa wito wa azimio ya utatuzi wa mgogoro unaotokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria, ikiwa ni pamoja na watu kulikimbia taifa hilo kwenda nchi jirani na kadhia ya ulanguzi wa dawa za kulevya eneo lote la kanda.

Akitoa tangazo hilo jioni ya jana Jumapili, Mkuu wa Umoja wa Mataifa ya Kiarabu, Ahmed Aboul Gheit amasema matarajio yake ni kwamba mataifa mengi ya magharibi yanaweza yasifurahishwe na uamuzi wao huo huo wa lakini huo ni uamuzi huru wa mataifa ya Kiarabu ambao unaona kwamba maslahi yao yanahitaji, kwa wakati huu mahususi, kutoliacha suala la Syria kwa namna lilivyoendelea kuwa.

Tangazo la uanachama kamili wa Syiria

Ägypten I Treffen der Arabischen Liga in Kairo
Washiriki wa mkutano wa mataifa ya Kiarabu wa CairoPicha: Amr Abdallah Dalsh/REUTERS

Kiongozi huyo aliongeza kwa kusema "Syria, kuanzia jioni hii, imekuwa mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa ya Kiarabu. Na kuanzia kesho asubuhi, wana haki ya kuchukua nafasi yoyote wanayostahili, na ikiwa wamealikwa na nchi mwenyeji, ambayo ni Ufalme wa Saudi Arabia kwa mkutano ujao wa kilele wa mataifa hayo ya Mei 19, Rais wa Syria Bashar al-Assad anaweza kushiriki."

Wakati mataifa ya Kiarabu ikiwa ni pamoja na Umoja wa Falme za Kiarabu kushinikizwa kusimamisha mara moja hatua ya kutengwa kwa Rais Assad, baadhi wamepinga hatua hiyo pasipo kuwepo kwa suluhu ya kisiasa kwa mgogoro wa Syria, ikiwa kama sharti muhimu la Syria kuridhiwa kurejea katika jumuiya hiyo.

Qatar, ambayo tangu awali ilikuwa inapingwa kuresjeshwa kwa Syria katika umoja huo ilisema msimamo wake juu ya kurejesha diplomasia na taifa hilo haujabadilika na ilitumai kwamba makubaliano ya kikanda kuhusu Syria yanaweza kuwa  na nia ya  kutoa msukumo kwa utawala wa Syria kushughulikia mizizi ya mgogoro.

Soma zaidi:Wakuu wa majimbo ya Ujerumani wanaishinikiza serikali ya shirikisho iongeze fedha za kuwahifadhi wakimbizi.

Itakumbukwa Novemba 2011, chombo hicho kilisimamisha serikali ya Damascus kutokana na ukandamizaji wake dhidi ya maandamano ya amani ambayo yalianza mapema mwaka huo na ambayo yalizidi kuwa mzozo ambao umeua zaidi ya watu 500,000, mamilioni ya watu kuyahama makazi yao na kuharibu miundombinu na viwanda vya nchi hiyo.

Vyanzo: RTR/AP/AFP