1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matarajio ya wengi kuhusu utawala wa Obama

Jane Nyingi19 Januari 2009

Barack Obama anaingia ikulu ya Marekani White House leo huku akikabiliwa na mzigo mkubwa wa matumani sio tu kutoka kwa wananchi waliomchagua wa marekani bali dunia kwa jumla.

https://p.dw.com/p/GcDJ

Jinsi atavyo shughulikia changamoto inayomkabili ndiko kutakakotoa sura ya mwelekeo wa utawala wake.Jane nyingi anayo zaidi.


Kura za maoni zahivi karibuni nchini marekani zinaonyesha kuwa Barack Obama anaingia madarakani akiwa na umaarufu mkubwa, kama alivyokuwa mrepublican Ronald Regan mwaka 1981.


Kwa mujibu wa mshauri mmoja wa zamani wa ikulu white house William Galston watu wengi duniani wamemchukulia Obama kama rais wao. Hii inaashiria matarajio walioko nayo ya mwamko mpya katika diplomasia ya marekani baada ya miaka minane ya uongozi wa rais George Bush ambaye wengi wanahisi utawala wake uliyangawanya mataifa badala ya kuyaleta pamoja na kusababisha hali ya wasiwasi.


Huku Bush akishtumiwa kwa kupuuza mgogoro wa muda mrefu kati ya Israel na palestina alipokuwa madarakani,Obama hajasita kuzungumzia swala hilo kwa njia ya kidiplomasia kutokana na Israel kuushambulia ukanda wa gaza.Swala la mashariki ya kati litakuwa changamoto kubwa kwa Obama


Otone Obama


Katika bara la ulaya kuna afeuni fulani kufuatia kumalizika kwa utawala wa rais Bush.Hata hivyo mshauri mmoja wa Obama amesema washirika wa marekani wa jumuiya ya NATO wanapaswa hivi sasa kuonyesha upendo,kwa kuongezeka idadi ya wanajeshi wake watakaokabiliana na wapiganaji wa kitaliban na wakundi la kigaidi la la-qaeda nchini Afghanistan.


Marekani ina karibu wanajeshi elfu 33 nchini Afghanistana na ina mipango ya kuwapeleka wanajeshi elfu 13 zaidi.Mataifa ya bara la ulaya ambayo ni wanachama wa NATO yanakaribu wanajeshi elfu 27 pekee nchini humo


Galston amesema Afghanistan itakuwa kama jaribio la kuonyesha jinsi Obama anayouungwa mkono na serikali za bara la ulaya,hasa ikizingatiwa baadhi ya mataifa ya bara hilo yanasita katika kuwachukua wafungwa walioko katika gereza la gurantanamo bay na hivyo kuchelewesha kufungwa kwake.


Licha ya Obama kutoa tahadhari kuwa serikali ya Pakistan inapaswa kutia juhudi zaidi dhidi wapiganaji wa kundi la al-Qaeda,matifa ya bara la ulaya yanaonekana kumuunga mkono rais aliyeko madarakani hivi sasa.


Mrepublican seneta Lindsey Graham alizungumza kuhusu umaarufu wa Obama baada ya kurejea Marekani kufuatia ziara yake na makamu wa rais mteule Joseph Biden nchini Iraq,Afghanistan na Pakistan,akisema:-


"Siwezi kueleza kiwango cha shauku niliyoishuhudia nchini Pakistan kuhusu rais mpya wa marekani Barack Obama,aliwaambia waandishi wa habari seneta Lindsey.


Nchini Marekani serikali ya Obama inatarajiwa kuufua uchumi uliodorora na kuwapa matumaini mamilioni ya wamarekani waliokuwa na wasiwasi wa kupoteza nafasi zao za ajira. Obama ataapishwa kushika hatamu hii leo.