1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matatizo ya uchumi duniani yahitaji ufumbuzi wa dharura

27 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CyJB

DAVOS: Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF,Dominique Straus-Kahn akizungumza katika Kongomano la Kiuchumi Duniani mjini Davos,Uswisi amesema,matatizo yanayokabili uchumi wa dunia ni makubwa na yanahitaji kupatiwa ufumbuzi.Akaongezea kuwa miongoni mwa hatua za kuchukuliwa ni kupunguza viwango vya riba na kuongeza matumizi ya serikali.Hofu ya kuporomoka kwa uchumi wa Marekani na katika nchi zingine pamoja na masoko ya hisa yanayoyumba yumba ni mambo yanayoathiri utabiri wa jumla wa hali ya uchumi mjini Davos.