1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mateka 455 wakombolewa na jeshi la Nigeria

Daniel Gakuba
14 Machi 2017

Kiasi ya mateka 455 waliokuwa wakishikiliwa na kundi la Boko Haram wamekombolewa na jeshi la Nigeria kwa mujibu wa msemaji wa jeshi hilo Sani Usman.

https://p.dw.com/p/2Z8b8
Nigeria Soldaten an einem Checkpoint in Gwoza
Picha: picture-alliance/AP Photo/L. Oyekanmi

Msemaji wa jeshi la Nigeria amesema wanajeshi wa nchi hiyo wamewakomboa watu 455 waliokuwa wakishikwa mateka na kundi la Boko Haram. Watu hao walikuwa wakizuiliwa katika vijiji vine kwenye wilaya ya Kala abalge Kaskazini Maskariki mwa jimbo la Borno, na sasa wamehamishiwa katika kambi ya wakimbizi katika mji wa Rann. Msemaji huyo, Sani Usman amesema magaidi wamewamiminia risasi wanajeshi wa serikali katika kijiji kimojawapo cha Kutila. Katika kijiji kingine cha Shirawa, wanajeshi waligundua kituo cha vifaa cha Boko Haram, zikiwemo fulana mbili zinazovaliwa na washambuliaji wa kujitoa mhanga. Tangu mwaka 2009, watu wasiopungua 14,000 wameuawa na kundi la Boko Haram, katika nchi za Nigeria, Chad, Niger na Cameroon. Kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa, wengine milioni 2.7 wameyakimbia makazi yao, kuepuka mashambulizi ya kundi hilo.