1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matokeo ya Kura ya Maoni Visiwani Zanzibar

2 Agosti 2010

Kura ya maoni iliofanywa Zanzibar, kuwauliza wananchi kama wanataka katiba ya nchi yao ibadilishwe ili kuweko serikali ya Umoja wa taifa baada ya uchaguzi mkuu ujao , asilimia 66.4 ya wapiga kura walisema wanaunga mkono.

https://p.dw.com/p/OZwX
Mji Mkongwe wa ZanzibarPicha: Stefan Pommerenke

Hiyo ina maana Baraza la Wawakilishi visiwani humo litakutana kuibadilisha katiba ya Zanzibar ili kuweka njia wazi ya kuweko serikali ya Umoja wa taifa, huenda sana baina ya vyama vya CCM na CUF.

Othman Miraji alizungumza punde hivi na mkuu wa upinzani katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hamad Mohammed, ambaye yumo katika uongozi wa Chama cha CUF, na pia Othman Miraji alizungumza na Harun Suleiman, waziri wa elimu wa Zanzibar, na mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama tawala cha CCM.