1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matokeo ya mwanzo yampa ushindi Rais Saakashvili

7 Januari 2008

---

https://p.dw.com/p/ClDL

TBILISI

Matokeo rasmi ya mwanzo katika uchaguzi war ais nchini Georgia yanaonyesha ushindi wa moja kwa moja wa rais Mikhail Saakashvili.Matokeo hayo yanampa ushindi wa asilimia zaidi ya 50 ya kura bwana Mikhail matokeo ambayo yanaweza yakaepusha kufanyika kwa duru ya pili ya uchaguzi.Hata hivyo mkuu wa tume ya uchaguzi nchini humo ameiambia Redio Deutsche Welle kwamba inaweza ikachukua hadi wiki mouja kwa matokeo ya mwisho kutangazwa.Maelfu ya wafuasi wa upinzani wanaandamana katika mji mkuu Tbilisi kupinga uchaguzi huo ambao wanadai umekumbwa na mizengwe iliyopangwa na rais.Waangalizi wa Ulaya lakini wamesema wameridhishwa na jinsi uchaguzi huo ulivyokwenda kwa njia ya huru na haki.