1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matokeo ya uchaguzi wa Israel si bayana

23 Januari 2013

Matokeo ya uchaguizi nchini Israel yamebainisha mwanya uliopo kati ya kambi mbili kubwa: Mrengo wa kati kushoto na kambi ya siasa kali za mrego wa kulia.

https://p.dw.com/p/17QGn

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amecheza bao na kushindwa.Hakufanikiwa,kwa kuitisha uchaguzi wa kabla ya wakati kupata ushindi madhubuti wa vyama vya mrengo wa kulia.Kinyume kabisa.Viti 31 tu ndivyo vilivyouendeya muungano wa vyama vya Likud na Israel Beiteinu-kasoro ya viti 11 ikilinganishwa na uchaguzi wa mwaka 2009.Na hata kambi yake,ikichanganyika na chama kipya cha siasa kali za mrengo wa kulia"Nyumba ya uyahudi" na vyama vyote viwili vya nadharia kali za kiorthodox,hawawezi kupindukia viti 60 kati ya viti 120 vya bunge la mjini Jerusalem.

Katika kambi ya mrengo wa kati-kushoto,idadi ya viti havipindukii 30-bila ya vyama vya waarabu-hakuna mageuzi ya kisiasa yatakayowezekana.Kuanzia chama cha Labour kinachoongozwa na Shelly Yachimowitsch hadi kufikia chama kipya cha waziri wa zamani wa mambo ya nchi za nje Tzipi Livni,vyote hivyo vilikuwa nyuma ya makadirio yaliyowekwa.Chama cha Kadima ambacho katika uchaguzi uliopita kilikamata nafasi muhimu,kimepwaya na kubakiwa pengine na viti viwili tu safari hii.

Turufu iko upande wa chama cha Jesch Atid

Mshindi bayana wa uchaguzi ni mtu ambae hataki kuelemea katika kambi yoyote ya kisiasa.Mtangazaji wa zamani wa televisheni Yair Lapid na chama chake cha Jesch Atid kinachomaanisha "Matumaini yapo."Hadi sasa amejikingia viti 19 na hivyo kugeuka kundi la pili kubwa katika bunge jipya la Israel-Knesset.Lakini ushindi wa Lapid ambae wazee wake ni mashuhuri na mwenyewe pia ni,mwandishi habari maarufu unadhihirisha kizungumkuti cha Israel:hakuna ajuaye anapigania nini hasa.Pengine hata yeye mwenyewe hajui.Katika kampeni za uchaguzi alikataa kata kata kujibu masuala bayana ya kisiasa.Hataki kuelemea kushoto wala kulia anasema anapigania usawa katika jamii,anapigania hali bora ya kiuchumi,anapinga rushwa na anataka watu waachane na mtazamo wa kale wa kisiasa.

Lakini karata ziko mikononi mwake yeye sasa Lapid.Anaweza kuchangia katika serikali ya muungano wa vyama vya mrengo wa kulia na kuongozwa na Benjamin Netanyahu au kuungana na makundi yasiyoelemea upande wa kidini .Na jambo hilo ndilo linaloweza kuzusha maajabu.Hata hivyo hata muungano kama huo hautasaidia kulifumbua tatizo sugu la nchi hiyo:yaani ufumbuzi wa mzozo wa mashariki ya kati.Hakuna hata chama kimoja kati ya vikuu kilichozungumzia katika kampeni za uchaguzi kuhusu kukomeshwa ujenzi wa makaazi mepya ya wahamiaji wa kiyahudi au kuzungumzia kuhusu ufumbuzi wa mzozo pamoja na wapalastina.Kwa wakati wote ambao wanasiasa watakwepa kulizungumzia suala hilo,wapiga kura hawatoweza kuzusha maajabu.

Mwanadishi:Marx,Bettina/Hamidou Oummilkheir

Mhariri: Josephat Charo