1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matokeo ya urais DRC kutolewa baada ya masaa 48

7 Desemba 2011

Kamisheni ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeahirisha kutangaza mshindi wa kinyag'anyiro cha urais kufuatia uchaguzi wa wiki iliyopita na kuzusha hofu ya kutokea kwa vurugu nchini humo.

https://p.dw.com/p/13Nzj
epa03018040 Electoral staff hold a meeting during presidential and parliamentary votes at a polling station in the capital Kinshasa, the Democratic Republic of Congo, 28 November 2011. Voting began despite concern of delay and violence while may voters complained of missing their names on the voters' list, late opening of polling stations and missing ballot papers. Seventy eight-year-old top opposition leader Etienne Tshisekedi of Democracy and Social Progress (UDPS) and Vital Kamerhe, a former UDPS member, are among many others who are challenging incumbent Joseph Kabila in the country's second election since the end of a bloody civil war in 2003. Election-related violence has already broken out in parts of the country and many predict that post-election violence is almost certain, if incumbent president declares victory. EPA/DAI KUROKAWA +++(c) dpa - Bildfunk+++
Masanduku ya kuraPicha: picture-alliance/dpa

Maafisa nchini humo wamedai wanahitaji muda mwingine zaidi ili kuweza kukukusanya matokeo ya mwisho, baada ya kutokea makosa katika usimamizi. Kutokana na hali hiyo matokeo kamili kwa hivi sasa yatategemewa alhamis jioni. Rais wa sasa Joseph Kabila mpaka sasa anaongoza kwa asilimia 46.4 ya kura katika theluthi mbili ya kura zilizoripotiwa kuhesabiwa. Mpinzani wake mkubwa Etienne Tshisekedi anamfuatia kwa asilimia 36.2. Vurugu za uchaguzi nchini humo zimesababisha vifo vya watu 18 na kujeruhiwa zaidi ya 100. Kwa mujibu wa makundi ya haki za binadamu vifo vingi vimetokana na jeshi la serikali.