1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matumaini ya Afrika katika miaka 50 ijayo

25 Mei 2013

Mataifa ya Afrika yanasherehekea miaka 50 tangu kuundwa kwa umoja wa nchi huru za Afrika , OAU, leo (25.05.2013)jumuiya iliyokusudiwa kuleta umoja wa bara hilo.

https://p.dw.com/p/18djK
Blick in den Konferenzraum im Afrika-Haus während der Eröffnung der Konferenz mit 31 afrikanischen Staats- und Regierungschefs am 22. Mai 1963. Am 25. Mai 1963 wurde in der äthiopischen Hauptstadt Addis Abeba die Organisation Afrikanischer Einheit (OAU) gegründet.
Kikaocha ufunguzi hapo tarehe 22, Mei 1963 na siku mbili baadaye OAU iliundwa.Picha: picture-alliance/dpa

Mfalme Haille selassie wa Ethiopia na wakuu wa nchi na serikali 31 walikutana mjini Addis Ababa tarehe 25, mwezi wa Mei kuizindua jumuiya hiyo mwaka 1963. Uzinduzi wa OAU , Umoja wa nchi huru za Afrika miaka 50 iliyopita unaadhimisha hatua muhimu ya kihistoria kwa bara zima, ambalo lilikuwa wakati huo likipitia kwa haraka katika kipindi cha kutoka katika ukoloni.

Mfalme Haille Selassie na viongozi wengine wa mataifa ya Afrika na serikali waliasisi umoja huo mjini Addis Ababa.

Eine Ehrenformation steht zum Empfang der ankommenden Konferenzteilnehmer auf dem Flughafen von Addis Abba. Am 25. Mai 1963 wurde in der äthiopischen Hauptstadt Addis Abeba die Organisation Afrikanischer Einheit (OAU) gegründet.
Gwaride la kuwakaribisha viongozi wa Afrika mjini Addis Ababa mwaka 1963Picha: picture-alliance/dpa

Makucha ya ukoloni

Wengi wa viongozi ambao walikuwapo wakati huo wameweza hivi karibuni tu kujitenga na hisia za kikoloni na wanatafuta njia kwa nchi zao kujenga upya mifumo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi iliyoporomoka kwa kutaka kushirikiana zaidi na majirani zao.

Upande wa kusini , makoloni ya Ureno ya Angola na Msumbuji bado yanakabiliwa na hali ya kujitoa kutoka katika zaidi ya muongo mmoja wa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

Hatua hiyo ni ndefu zaidi kwa hali ya baadaye ya Zimbabwe na Namibia, ambapo nchi hiyo ilikuwa inadhibitiwa na Afrika kusini ya kibaguzi wakati huo, na ilichukua zaidi ya miaka 30 kabla ya Afrika kusini binafsi kufikia serikali ya kidemokrasia.

Maadhimisho

Mkusanyiko huu wa kihistoria leo(25.05.2013) ni ishara ya ndoto za bara ambalo limenyonywa vya kutosha.

Kwa Waafrika wengi ndoto hizo bado hazijatimia licha ya matumaini ya muda huo na juhudi kubwa tangu wakati huo.

Der äthiopische Kaiser in einer undatierten Aufnahme. Kaiser Haile Selassie wurde am 23. Juli 1892 in Edjersso als Prinz Tafari Makonnen geboren. Am 2. November 1930 ließ er sich zum Kaiser krönen. Nach dem erfolgreichen Abessinien-Feldzug der Italiener floh er 1936 ins britische Exil, kehrte jedoch 1941 mit britischen Truppen zurück und zog am 5. Mai 1941 wieder in Addis Abeba ein. Innenpolitisch nicht sehr erfolgreich, verfolgte er eine rege Reisediplomatie. Die Gründung der "Organisation für afrikanische Einheit" (OAU) im Mai 1963 in Addis Abeba war hauptsächlich sein Werk. Anfang Juli 1974 übernahmen die Miltärs die Macht und setzten ihn am 12. September 1974 formell als Kaiser ab. Die folgenden Jahre verbrachte Haile Selassie unter strengem Hausarrest im Menelik-Palast in Addis Abeba, wo er am 27. August 1975 starb, wobei sich stets die Vermutung hielt, das er einem Mordanschlag zum Opfer gefallen war.
Marehemu mfalme Haile Selassie wa EthiopiaPicha: picture-alliance / dpa

Katika hotuba yake kwa viongozi waasisi wa OAU, Haille Selassie alikumbusha udhalilishaji uliofanyika hapo kabla.

"Kipindi cha ukoloni ambacho tulitumbukizwa , kilitufikisha mahali bara hili kudhibitiwa na wakoloni , na watu wetu ambao walikuwa huru na wenye kujisikia fahari kudhalilishwa na kuwa watumwa." amesema.

"Leo Afrika imejitokeza kutoka katika njia hii ya giza. Mapambano yetu dhidi ya uovu yamekwisha.

Hali hii ilikuwapo katika baadhi ya sehemu za Afrika, ikiwa ni pamoja na Ethiopia yenyewe.Mfalme alitangaza kuwa bara hilo liko njiani kati ya Afrika ya kale na Afrika ya hapo baadaye. Wengi wangesema kuwa hali hiyo bado imeendelea hata baada ya miaka 50.

epa03084113 A handout image made available by the South African Government Communication and Information System (GCIS) shows a general view of the the new African Union building where the present 26th meeting of the NEPAD Heads of State and Government Orientation Committee (HSGOC) is being held, Addis Ababa, Ethiopia, 29 January 2012. EPA/Jacoline Prinsloo / GCIS / HANDOUT HANDOUT EDITORIAL USE ONLY/NO SALES
Viongozi wa sasa wa Umoja wa Afrika mjini Addis AbabaPicha: picture-alliance/dpa

Waafrika wengi bado wana uhaba wa chakula na wanaishi katika umasikini uliokithiri. Mabadiliko ya hali ya hewa yameleta ukame na mafuriko. Ukosefu wa ajira ni mkubwa, huku kukiwa na matumaini machache kwa vijana katika maeneo mengi ya bara hilo.

Vita na mizozo

Mapigano yanaendelea nchini Mali, jamhuri ya kidemokrasi ya Congo na Sudan.

Libyan leader Moammar Gaddafi attends the opening of the African heads of State summit in Addis Ababa, Ethiopia on 02 February 2009. African heads of states and governments designated the Libyan leader Moammar Gaddafi to chair the African Union for one year. Gadhafi's election at the head of the African Union could give Libya the opportunity to follow closely the ongoing efforts to organize peace talks between Sudan government and Darfur main rebel movements EPA/SABRI ALMHEDWI +++(c) dpa - Report+++
Marehemu Muammar GaddafiPicha: picture-alliance/ dpa

Wanadiplomasia wa Afrika wanasema mradi wa kuiunganisha Afrika kuwa bara lenye amani si jambo lililoshindwa lakini ni hatua inayoendelea.

Umoja wa Afrika, AU ulianzishwa mjini Durban mwaka 2002 kuchukua nafasi ya Umoja wa nchi Huru za Afrika, OAU, kwa msukumo wa kiongozi wa zamani wa Libya Moammar Gaddafi.

United Nations troops patrol on the road to Sake, 27kms from the provincial capital of Goma, in the Democratic Republic of the Congo, on 04 November 2008. The United Nations and international aid organization are fighting an uphill battle to get help to over 250,000 people that are thought to have been forced from their homes and villages. EPA/STEPHEN MORRISON +++(c) dpa - Report+++
Wapiganaji wa M23 katika jamhuri ya kidemokrasi ya CongoPicha: picture-alliance/dpa

Wazo la umoja mara nyingi lilishindwa kwa msingi wa kutotaka kujiingiza katika masuala ya ndani ya nchi nyingine huru, OAU ilikuwa haina nguvu kabisa kutokana na mapinduzi ya kijeshi , vita vya wenyewe kwa wenyewe na hata mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994.

Mwandishi . Sekione Kitojo / dpae

Mhariri: Abdu Mtullya