1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matumaini ya Bush juu ya amani mashariki ya kati ni ya kweli?

10 Januari 2008

---

https://p.dw.com/p/CnGA

JERUSALEM

Rais George W Bush aliyeko ziarani mashariki ya kati amewatolea mwito Wapalestina na waisrael kuchukua nafasi hii ya kihistoria kujaribu kupata amani katika eneo hilo.Kwenye mkutano na waandishi habari pamoja na waziri mkuu Ehud Olmert rais Bush amesema anamatumaini kwamba huenda makubaliano ya amani yakapatikana kufikia mwishoni mwa mwaka.Lakini amesema hilo linawezekano tu ikiwa wapalestina na waisrael watakubaliana juu ya masuala tete yaliyopo.

Kwa upande mwingine waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert amesema amani haiwezi kupatikana kati ya waisrael na wapalestina ikiwa wanamgambo wa kipalestina wataendelea kufanya mashambulizi dhidi ya Israel.Palestina inasema ikiwa rais Bush anataka kusaidia kweli kuleta amani baina ya pande hizo mbili lazima awabinye waisrael wakomeshe ujenzi wa makazi ya walowezi wa kiyahudi katika maeneo yote ya ardhi ya wapalestina. Ziara ya Bush imekaribishwa na mashambulio ya roketi kutoka upande wa Gaza pamoja na mashambulio ya anagani ya kulipiza kisasi kutoka Israel,hali ambayo inayafanya mazungumzo ya kutafuta amani kuwa magumu.