1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matumaini ya kumalizwa mzozo wa kisiasa Kenya

22 Februari 2008
https://p.dw.com/p/DBS7

NAIROBI:

Kuna ishara kuwa maendeleo yamepatikana katika mazungumzo yanayofanywa nchini Kenya kati ya serikali na chama kikuu cha upinzani cha Raila Odinga- ODM.Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan anaesimamia mazungumzo hayo,pande hizo mbili zimekubali kuanzisha wadhifa wa waziri mkuu ukitegemewa kushikwa na Raila Odinga.

Vile vile majadiliano yataendelea kuhusu madaraka ya Rais Mwai Kibaki. Zaidi ya watu 1,000 wameuawa na maelfu wengine wamepoteza makaazi yao katika machafuko yaliyozuka nchini humo kufuatia uchaguzi wa Desemba 27 uliomrejesha madarakani Rais Kibaki.