1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matumaini ya walimwengu yaelekezwa Annapolis

25 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CSu0

Washington:

Kiongozi wa Utawala wa ndani wa Palastina Mahmoud Abbas amewasili Marekani kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa Mashariki ya kati utakaoanza jumanne ijayo huko Annapolis karibu na Washington.Akiwa njiani kuelekea Washington rais mahmoud Abbas amewaambia waandishi habari tunanukuu:”Nimekuja Annapolis kujaribu kutekeleza mahitaji na ndoto ya umma wa Palastina ya kua na taifa lao”Mwisho wa kumnukuu kiongozi wa utawala wa ndani wa Palastina aliyezungumzia matumaini kuona mazungumzo ya Annapolis yakipüelekea kutekelezwa maazimio ya kimataifa,utaratibu mpya wa amani unaosimamia na pande nne,juhudi za nchi za kiarabu na dhamiri za rais Bush za kuwepo madola mawili-Israel na Palastina.Kwa upande wake waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert akiwa njiani kuelekea Annapolis ameelezea matumani yake ya kuona mkutano huo wa kimataifa ukifungua njiani ya kuanzishwa mjadala wa dhati kuhusu masuala ya kimsingi kati ya Israel na Palastina.Jumuia ya nchi za kiarabu imeamua kushiriki katika mkutano wa kimataifa wa Annapolis unaosimamiwa na rais George w. Bush wa Marekani.