1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matumizi ya nguvu Gaza.

Mutasa Omar28 Mei 2007

Jeshi la Israel sasa limepewa madaraka zaidi ya kuongeza vikosi vyake vya ardhini kupambana na wapiganaji wa Hamas ndani ya Gaza

https://p.dw.com/p/CHDg
Jengo la wapalastina lateketezwa.
Jengo la wapalastina lateketezwa.Picha: AP

Hii imefatia ufyatuaji wa makombora ya Qassam jana, yaliomuawa raia moja wa Israel katika mji wa Sderot.

Tangu mapigano haya yaanze karibu siku kumi na mbili zilizopita, wapalastina zaidi ya Arubaini wamesha uwawa, wengi wao wakiwa wapiganaji wa Hamas.

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert amesema ameliamrisha Jeshi la Israel kufanaya kila njia kuzuwia mashambulizi ya wapiganaji wa kundi la Hamas. Waku wa jeshi la Israel wanasema sasa idadi ya wanajeshi wa Ardhini itaongezwa ili kuingia mji wa Ghaza kuviteketeza vituo vya wapiganaji wa Hamas vinavyotumiwa kurushia makombora dhidi ya Isarel.

Uamuzi huu ulichukuliwa baada ya waziri mkuu Ehud Olmert kukutana na waziri wake wa ulinzi Amir Peretz pamoja na mkuu wa jeshi la Israel, Lt Gen Gabi Ashkenazi.

Hata hivo Bw Olmert ameliambia Bunge lake kua wasitarajie suluhisho la mapema kuwamaliza wapiganaji wa Hamas dhidi ya Israel .na pia akaonya kua Israel haitokubali shinikizo lolote kutoka njee ili ikomeshe mashambulizi yake dhidi ya Hamas.

Bw Olmert alisema na mnukuu; Hapatokueko kikomo kupambana na makundi haya ya kigaidi, wala hao wanaohusika na makundi hayo, hakuna atakae salimika. Mwisho wa kumnukuu. Wanajeshi wa Israel leo wamewapiga risasi wapiganaji wawili wa Hamas na kuwajeruhi vibaya, viongozi wa Hamas wamethibitisha habari hizo.

Hadi kufikia sasa wapalastina zaidi ya hamsini, wengi wao wakiwa wapiganaji wa Hamas wameuwa na mashambulizi ya ndege za kivita za Israel tangu Israel ianze mashambulizi yake siku kumi na mbili zilizopita.

Hapo jana Hamas walivurumisha makombora zaidi ya 9 katika mjii wa Sderot kusini mwa Israel na kumuuwa mtaalam moja wa mambo ya kompyuta alipokua akiendesha gari lake.

Hii ni mara ya pili kwa kipindi cha week moja makombora ya wapiganaji wa Hamas kumuuwa mtu wa pili, raia wa Isreal, na leo Asubuhi makombora matatu yalivurumishwa katika mjii huo wa Sderot, na inasemekana mtuu moja amejeruhiwa .

Wakati huo huo chama cha Labour nchini Israel leo kinamchagua kiongozi wake, na wagombea walijitokeza ni Ehud Barak aliewai kua waziri mkuu wa Israel akichuana na Ami Ayalon, aliwai kua mkuu wa kikosi cha upelelezi cha Shin Beth, pamoja na waziri wa ulinzi wa Israel, Amir Peretz ambae kwa sasa ndie kiongozi wa chama cha Labour.

Ikiwa hakuna atakae pata sichini ya 40 ya kura, basi itafanyika duru ya pili tare 11 mwezi June.