1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matumizi ya nguvu wageni

4 Januari 2008

Adhabu kali zimedaiwa wachukuliwe vijana wa asili ya kigeni nchini Ujerumani kwa vitendo vyao vya uhalifu:

https://p.dw.com/p/CkOC

Mjadala umeuma moto nchini Ujerumani kuhusu wageni waishio humu nchini wanaotumia nguvu na jinsi mada hii inavyotumiwa katika kampeni za uchaguzi ujao.

Mzee mmoja wa miaka 76 aliwaomba vijana 2 wa kigeni katika eneo la reli ya chini ya ardhi-Underground- wazime sigara zao waliozokuwa wakivuta.Badala ya kuzima walim kashifu huyo mzee na wakaanza kumpiga tena kikatili kabisa.

Vijana hao ni mturuki mwenye umri wa miaka 20 na mgiriki wa umri wa miaka 17.

Waziri mkuu wa mkoa wa Hesse Roland Koch anadai sheria za uhalifu kwa chipukizi zizidishwe makali .Hatahivyo, mwito wake unaonekana si chochote zaidi ya jaribio la kampeni ya kujipatia kura muda mfupi kabla ya uchaguzi wa mkoa wake wa Hesse.

Bw.Roland Koch anaelewa vyema jinsi gani kushinda uchaguzi kwani lengo lake ni kubakia tena madarakani mwezi huu baada ya uchaguzi wa jimbo la Hesse.

Uchunguzi wa maoni unabainisha an ashindwa.Mhafidhina huyu kwahivyo, ameamua kutumia biramu hilo la sheria kali kwa wageni kujipatia kura –uhalifu miongoni mwa vijana wa asili ya kigeni nchini Ujerumani ni mada ya uchaguzi.

Lakini, mada hii sio tu si mpya, bali ni sehemu tu ya balaa zima lililoikumba jamii.

Bw.Koch ameitisha vijana au watoto wageni wanaotumia mabavu nchini Ujerumani wanabidi kupewa adhabu kali.

Kwamba mwanasiasa huyu wa chama cha CDU amechagua kipindi cha kutokuwapo habari motomoto-kutoa dai lake ni janja yake.

Ni nadra katika kipindi i cha X-masi na kuamkia mwaka mpya kwa mwanasiasa kupasua bomu kama hilo la kisiasa.Katika sera za ndani Ujerumani kwahivyo tangu siku kadhaa sasa kinachozungumzwa na matamshi ya Bw.Roland Koch.

Mjadala aliouzusha lakini haukuchangia chochote hadi sasa kulitatua tatizo lililozuka.Kinyume chake: Mabawa ya shoto na kulia yameanza kupambana .

Ukweli wa mambo ni kuwa, vijana wa kigeni humu nchini waliotayari kutumia nguvu ni wachache tu katika jamii .sasa kuligeuza hili kuwa tatizo linalozushwa na wageni humu nchini ni kutia chumvi.Ukilinganisha vijana chipukizi wa kijerumani wanaotumia mabavu na wale wa kigeni tofauti ni kubwa.

Kuponesha jaraha hili kuna wanaodai adhabu kali lakini wako pia miongoni mwa wanasiasa wanaodai kuchukuliwa hatua za kusaidia jamii ya wageni na shida zao ili kuwakomboa vijana kama hao wanaotumia nguvu na sio kuwachukulia zaidi adhabu kali.

Kwani, matumizi ya nguvu n a uhalifu unaitapakaa zaidi miongoni mwa chipukizi na hasa vijana wakiume nchini Ujerumani ni tatizo la tabaka ya chini na kwa jicho la pili ndio linakuwa tatizo la vijana wa kigeni au waliohamia nchini.

Siasa ya Ujerumani ya kuwajumuisha raia wa kigeni na jamii ya kijerumani kwa kadiri kubwa haikufanya kazi na mfumo wa elimu humu nchini unazidisha mwanya uliopo tangu kindergarten na kuwaweka watoto wa asili ya kigeni daraja ya chini.

Kwahivyo, kuchukua hatua za kuwasafirisha nchini kuwarudisha makwao pamoja na adhabu kali hakutasaidia kutibu maradhi yaliopo. Mfano wa Marekani unafaa hapa kuamngaliwa:

Magereza yake yamesheheni wafungwa na adhabu kali hadi za fifo hazikusaidia kuifanya miji ya marekani kuwa na usalama zaidi.Kinyume chake.

Kwa ufupi, baadhi ya mada zinazotumiwa katika kampeni ya uchaguzi ni kali mno,za zamani na zatatanisha kuweza kuzitumia kwa manufaa ya kisiasa.Januari 27 ikiwadia –siku ya uchaguzio mkoani Hesse,majada huu nao utatoweka,lakini tatizo lake litabakia pale pale hata baada ya uchaguzi huo.