1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matumizi ya Nguvu yamekithiri Jamhuri ya Afrika kati

6 Mei 2014

Wanajeshi wa kulinda amani wa Ufaransa wamewauwa wanamgambo kadhaa ,baada ya kuhujumiwa na watu kama 40 waliokuwa na silaha katika eneo la kakazini magharibi ya Jamhuri ya Afrika Kati.

https://p.dw.com/p/1BudT
Wanamgambo wa Anti Balaka wanaolidhibiti eneo la Nanga-BoguilaPicha: SIA KAMBOU/AFP/Getty Images

"Wanajeshi wa Ufaransa wanaotumikia opereshini Sangaris,walishambuliwa na wanamgambo kama 40 hivi waliokuwa na silaha" amesema Gilles Jaron mjini Paris."Mapigano yamedumu masaa matatu na baadhi ya wanamgambo wameuliwa,wamejeruhiwa na baadhi ya silaha zao kuharibiwa.Wengine wametoroka,"Amesema.

Jaron aliyekwepa kusema waasi wangapi hasa wameuliwa,amesema tu kwamba wanajeshi wao waliarifiwa kabla kwamba watui waliobeba silaha wanaelekea Boguila umbali wa kilomita 450 kaskazini ya mji mkuu Bangui.Hakuna mwanajeshi wa Ufaransa aliyejeruhiwa.

"Mapigano yalikuwa makali.Waasi walionyesha wamedhamiria kukiteka kituo cha kijeshi cha Ufaransa.Tulilazimika kuomba msaada wa ndege mbili za kijeshi.Makombora dhidi ya vifaru na mizinga pia ilitumika-"Wanajeshi wa Ufaransa walikuwa wanapiga doria katika eneo la kati ya mji wa Bossangoa na Paoua-eneo lililoko katika ncha ya kaskazini magharibi ya jamhuri ya Afrika.

Mapigano yalisita usiku ulipioingia.Na kwa mujibu wa duru za kuaminika,hali ilikuwa shuwari usiku kucha huku wanajeshi wa opereshini Sangaris wakiendelea kupiga doria katika maeneo ambayo wanajeshi wa Afrika wanaotumikia kikosi cha kimataifa cha MISCA waliyahama.

Vikosi vya Ufaransa na vile vya Afrika havikufanikiwa bado kurejesha utulivu

Shirika la Madaktari wasiokuwa na Mipaka-MSF limesitisha shughuli zake zote isipokuwa za dharura tu likilalamika dhidi ya kushindwa serikali kulaani kisa cha kuuliwa watu 16 katika vituo vyake vya matibabu huko Boguila,siku 10 zilizopita.

Zentralafrikanische Republik Ärzte ohne Grenzen in einer Klinik in Bangui
Watumishi wa shirika la madaktari wasiokuwa na Mipaka wakiendesha shughuli zao mjini BanguiPicha: SIA KAMBOU/AFP/Getty Images

"Pengine ni kundi hilo hilo la wanamgambo lililofanya mauwaji hayo"-msemaji wa jeshi la Ufaransa Gilles Jaron amesema.

Maelfu ya wanajeshi wa Ufaransa na wenzao wa kiafrika wameshindwa kuzuwia wimbi la mapigano ya kikabila yaliyoripuka baada ya waasi wa Seleka kutwaa madaraka katika jamhuri ya Afrika Kati,mwezi Marchi mwaka jana.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Reuters/AFP

Mhariri:Yusuf Saumu