1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mauji ya halaiki Rwanda

Sudi Mnette8 Aprili 2009

Mauji hayo ya halaiki yangeweza kuzuiwa

https://p.dw.com/p/HT78
Mmoja wa manusura wa maujia ya halaiki Rwanda.Picha: AP

Miaka 15 iliyopita wakati mitaa ya Rwanda iliposheheni maiti, ulimwengu ulifumba macho, ingawa vikosi vya kimataifa vya kulinda amani vilikuwa nchini humo. Lakini Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilivikataza vikosi hivyo kuingilia kati.


Tangu kumalizika kwa mauaji hayo ya halaiki, wataalamu wanachunguza mchango wa mataifa mengine ulimwenguni katika kuyadhibti mauwaji hayo, na tangu wakati huo ni wazi kuwa mauwaji yale ya halaiki yangeweza kuziliwa na idadi ya wahanga angalau yangepungua. Kwani, kabla mauwaji haya kutokea kulikuwa na ishara nyigi kwamba tukio hilo lingetokea


“Umoja wa Mataifa , New York. Kumeonekana kuongezeka mno kwa maandamano ya matumizi ya nguvu, mashambulio ya usiku ya makombora pamoja na mauwaji yaliochochewa na chuki za kikabila.

Kuna ushaidi kwamba, vikundi vyenye silaha vimeanza kurundika silaha zao tayari na pia vinataka kuzigawa kwa wafuasi wao. Hii ikitokea hali ya usalama itadhofika. Itakuwa tisho kubwa kwa hali ya usalama kwa wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa na raia hapa nchini.”


Miezi miwili kabla ya kutokea kwa mauwaji ya halaiki, mtaalamu wa Umoja wa Mataifa huko Rwanda Jacques-Roger Boo-Boo alituma ujumbe akiwa amekata tama. Hii ni moja kati ya vidokezo vingi ambavyo vilionyesha vile hali ilivyokuwa. Kikosi cha walinda amani cha Umoja wa Mataifa kilikuwa nchini Rwanda tangu mwisho wa mwaka 1993. Mashambulishi dhidi ya Watutsi, habari juu ya ufikishaji wa silaha kwa Wahutu, kambi za siri za mazoezi za wanamgambo, yote haya yaliripotiwa na kikosi cha umoja wa mataifa. Pia kulikuwa na taarifa zingine.

“Serikali ya Ubelgiji ilikuwa inajua kuhusu hatari iliyokuwepo na ikawafahamisha Marekani na Uingereza pamoja na wanadiplomasia wa Umoja wa mataifa kwamba ingetaka kuongeza idadi ya vikosi vya kulinda usalama. Marekani na Uingereza zilikataa kwasababu ya fedha. Hii Ilikuwa ishara mbaya kwa wale waliokuwa wamepanga mauwaji haya: walijuwa kuwa wangeweza kuyafanya na ulimwengu haungefanya kitu.”

Hivyo ndivyo asemavyo mwandishi Linda Melvin katika kitabu chake “A people betrayed: The role of the West in Rwanda's Genocide” , yaani Kuendewa kinyume umma-mchango wa magharibi katika mauaji ya hailaiki nchini Rwanda- ambaye alivichunguza vitendo vya mataifa ya magharibi katika tukio hilo na ambaye pia alitoa ripoti ya kitaalamu katika Mahakama ya kitaifa juu ya Ruanda. Wakati mauwaji ya halaiki yalipotokea hapo Aprili 7 mwaka wa 1994, vikosi vya kimataifa vya kulinda amani vilikukodoa macho tu. Mbele ya macho yao waziri mkuu alitekwa nyara na akauliwa. Watutsi 3000 walikimbilia kituo cha kikosi cha jeshi la Ubelgiji. Lakini wanajeshi wa Ubelgiji walipoanza kuuliwa, jeshi hilo liliondoka nchini. Watutsi wakabakia bila kinga na muda mfupi baadaye wanamgambo Wakihutu waliwauwa. Si Umoja wa Mataifa wala nchi yeyote ile, ilijaribu kuingilia.

“Badala yake ulimwengu ulijishughulisha na ile iliyokuwa Yugoslavia. Mauwaji ya halaiki yalipotokea Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na vyombo ya habari vya nchi za magharibi vilijishughulisha na matukio ya Balkan. Rwanda haikuwa na umuhimu kwa Umoja wa Mataifa na magazeti ya magharibi. Hata wakati shirika la kimataifa la misaada la “Oxfam” lilipoongea mara ya kwanza Apirili 29. kuhusu mauwaji ya halaiki nchini Rwanda, hakuna gazeti lilioandika habari hii. Kwa hivyo ilikuwa kushindwa kwa wanasaiasa na vyombo vya habari.

Vikosi vya Umoja wa Mataifa vilifanya juhudi ilipofika wakati wa kuwasafirisha wakaazi wakigeni kutoka nchini humo. Wakati huo huo kamanda wa vikosi vya Umoja wa Mataifa alivishinikiza vikosi hivyo vizuie mauwaji ya halaiki. Lakini, Baraza la Usalama halikusaidia naye hakuweza kufanya chochote. Hakupewa mamlaka ya kuvingoza vikosi hivyo kupambana na mauwaji hayo. Wanasiasa wa nchi za magharibi hawakutumia neno “mauwaji ya halaiki” hata mara moja. Bill Clinton aliyekuwa rais wa Marekani wakati huo, alisema vilikuwa vita vya kikabila. Koffi Annan ambaye baadae alikuwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa, alikuwa wakati huo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kama kiongozi wa vikosi vya kuhifadhi amani ni kati ya watu wachache ambao baadaye walijitwika dhamana.

“Hatutakiwi katu kusahau kwamba sote tulishindwa kuwalinda watu 800,000 wanaume, wanawake na watoto nchini Rwanda. Lazima tuchukuwe dhamana kuwa hatukufanya bidii ili kuzuia mauwaji haya ya halaiki.”

Hata hivyo, baadhi ya wachunguzi ulimwenguni, wanailaumu jumuiya ya kimataifa kuwa halijapata funzo kutoka darasa la Rwanda. Generali Romeo Dallaire kamanda wa zamani wa kikosi cha kuhifadhi amani cha Umoja wa Mataifa anazilaumu nchi za magharibi kuwa zinatazama tu mauwaji mengine ya halaiki yakiendelea- akimaanisha matukio huko Dafur.