1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mauritius:Wanawake wachache wawakilishwa serikalini

P.Martin17 Septemba 2008

Mauritius pamoja na Botswana,Malawi na Madagascar hazikusaini waraka wa usawa wa jinsia wakati wa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika-SADC mwezi Agosti.

https://p.dw.com/p/FKAd

Wakati kisiwa hicho kidogo cha bahari ya Hindi kimepiga hatua ya maendeleo fulani hivi karibuni katika uwakilishi wa wanawake kwenye ngazi zote bungeni.Lakini bado kuna mengi yakufanywa ili kuwaruhusu wanawake kuwa na haki zao kamili katika uwanja wa kisiasa. Mauritius inatazamiwa kusaini waraka au protokali hiyo ya usawa wa jinsia, ikiwa na azma ya kufikia lengo lake la asili mia 30 ya uakilishi wa wanawake katika ngazi zote serikalini ifikapo 2015.

Mwezi Julai 2005, vyama vitatu shirika vinavyoendesha shughuli za serikali nchini humo,Social Alliance cha Waziri Mkuu Navin Ramgoolam,Militant Movement of Mauritius cha Paul Berenger na Militant Social Movement, chama cha Pravind Jugnauth viliwateuwa wagombea 13 tu wanawake kati ya jumla ya wagombea 180 walioshiriki katika uchaguzi.

12 kati ya wanawake hao walichaguliwa na wawili waliteuliwa kuwa mawaziri. Sheilabai Bappoo ni Waziri wa Usalama wa Jamii na Mshikamano wa Kitaifa na Indira Seebun ni Waziri wa Wanawake na Ustawi wa Familia.Kalyanee Juggoo akateuliwa kuwa Naibu wa kiongozi wa serikali bungeni.Lakini wanawake hawa wanawakilisha sehemu ndogo ya wanawake nchini Mauritius ambao wamepigania kuendelea na shughuli za kisiasa.

Wanawake wako mstari wa mbele wakati wa kampeni za uchaguzi nyumba hadi nyumba pamoja na kuandaa mikutano na kugawa karatasi zinazoelezea muongozo wa vyama vyao,bila kusahau kujitolea kwao kuwapikia kuanzia wagombea,madalali wa vyama,hadi maafisa wengine.Hata hivyo,si wengi wanaojitokeza kuomba kuwa wagombea.

Lakini kuna kikwazo.Ingawa wengi wanahamu ya kujihusisha na siasa , hata hivyo si wengi miongoni mwa wanawake wa Kihindu na Kiislamu, waliotayari kuacha nafasi zao katika jamii ziathirike na kuharibiwa kwa kuonekana vyengine.Katika kisiwa hicho cha Mauritius viongozi wa jamii ya waislamu huwawekea vikwazo wanawake kuingia siasa kwa sababu ya mtazamo finyu wa mwanamke katika jamii.

Kwa Wahindu pia hali ni sawa na hiyo.Mwa mfano mwanamme mmoja alisikika akiuliza „ Vipi tunaweza kuwaruhusu wanawake wetu kupanda juu ya lori na kuwahutubia maelfu ya wanaume katika mkutano wa hadhara ?"

Ama Waziri Seebun aliea katika siasa kwa miaka 13 sasa anasema,yeye haoni kama kuna ubaguzi dhidi ya wanawake katika ngazi yoyote,ila ni wao wenyewe wenye kusita sita. Akaongezea,lazima wajitokeze.Ametaja mafanikio ya uakilishi wa wanawake katika nyanja mbali mbali .Kuna wanawake kadhaa wanaoongoaza idara za vyuo viku na kuna naibu mkuu wa chuo ambaye ni mwanamke.

Wakati Mauritius inajiandaa kusaini waraka juu ya usawa wa jinsia wa SADC, macho yanaelekezwa katika uchaguzi ujao 2010.Je, nini itakua nafasi ya wanawake katika uchaguzi huo ?