1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mauwaji ya Dendermonde Ubeligiji

Oumilkher Hamidou24 Januari 2009

kijana aliyeuwa akabiliwa na mashtaka

https://p.dw.com/p/GfLF

Brussels:


Mwendesha mashtaka wa  Dendermonde nchini Ubeligiji ameamuru  atiwe korokoroni kijana mwenye umri wa miaka 20 aliyemwaga damu katika shule moja ya chekechea katika mji huo.Kijana huyo anakabiliwa na mashtaka ya kuwauwa watu watatu na kufanya majaribio kadhaa ya kutaka kuuwa.Mtuhumiwa huyo amewachoma visu watoto wawili wadogo na mlezi wao.Kijana huyo amekataa  hapo awali kusema chochote kuhusu mauwaji hayo.Kwa mujibu wa maafisa wa polisi,kijana huyo alikua na akili zake,hakuwa amelewa wala kuvuta bangi alipoivamia shule hiyo ya chekecheya na kuanza kuchoma watu visu.