1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mavazi yanayopaswa kuvaliwa na wanasheria nchini Kenya

24 Januari 2013

Nchini Kenya chama cha wanasheria kimetangaza namna mpya ya mavazi yanayopaswa kuvaliwa na wanasheria nchini humo.

https://p.dw.com/p/17QgA

Wanasheria wote wa kike wamekatazwa kuvaa nguo zinazowabana na zinazoonesha miili yao, kutovaa nguo fupi na hata mitindo ya nywele ya rasta.

Wanasheria hao wametakiwa kuvaa nguo za heshima na kubakia na nywele zao bila ya kuziweka rangi ya aina yoyote.

Wanasheria wa kiume nao wametakiwa kuvaa suti za rangi nyeusi, kutovaa viatu vinavyoonyesha vidole na kuweka rasta ikiwa kuna baadhi ambao wana nywele za aina hiyo.

Chama cha wanasheria kinasema kimefanya hivyo ili watu walio na taaluma kama hiyo waheshimike na wawakilishe watu wakiwa wamevalia mavazi ambayo yanakubalika na jamii.

Amina Abubakar amezungumza na Bobby Mkangi ambaye ni wakili nchini Kenya na Mwanzo anatoa maoni yake juu ya aina hii mpya ya mavazi kwa mawakili ambayo tayari imeshaanza kufanya kazi nchini Kenya. Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Amina Abubakar

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman