1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri Rice na Miliband nchini Afghanistan

8 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D4DN

KABUL:

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Condoleezza Rice amesisitiza kuwa maendeleo yamepatikana nchini Afghanistan licha ya uasi wa Wataliban unaoendelea katika nchi hiiyo.Alikuwa akizungumza mbele ya wanajeshi na waandishi wa habari wakati wa ziara yake katika mji mkuu wa Afghanistan,Kabul. Vile vile Rice na Waziri wa Nje wa Uingereza David Miliband walikuwa na majadiliano pamoja na Rais wa Afghanistan Hamid Karzai.Kiongozi huyo wa Afghanistan ametetea uongozi wa serikali yake na akakanusha ripoti kuwa alivikosoa vikosi vya Uingereza vilivyopo nchini Afghanistan.Amesema,matamshi yake yamechukuliwa kinyume na muktadha.

Hapo awali Rice na Miliband walitembelea Wilaya ya Kandahar kusini mwa Afghanistan na walikutana na wanajeshi wa Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi NATO wanaopigana dhidi ya wanamgambo wa Kitaliban.