1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa ulinzi wa NATO wakutana Brussels

10 Oktoba 2012

Mawaziri wa ulinzi wa NATO na mataifa 22 wanakutana mjini Brussels kutathmini muongozo wa juhudi zao za kulisaidia jeshi la Afghanistan,vikosi vya ISAF vitakapoihama nchi hiyo mwaka 2014.

https://p.dw.com/p/16NXd
Waziri wa ulinzi wa Marekani Leon Panetta (kulia) na katibu mkuu wa NATO RasmussenPicha: Reuters

"Tunakutana ili kuthibitisha tutaendelea na jukumu letu kuhakikisha utulivu na hali iliyo imara nchini Afghanistan" amesema katibu mkuu wa jumuia ya kujihami ya NATO,Anders Fogh Rasmussen alipofungua mkutano huo katika makao makuu ya NATO mjini Brussels.

Wakati wa mkutano huo,mawaziri hao wa ulinzi wamearifiwa  kuhusu kuteuliwa kiongozi mpya wa kikosi cha kimataifa kinachoongozwa na NATO nchini Afghanistan-ISAF,jenerali wa kimarekani Joseph Dunford,badala ya jenerali John Allen aliyekuwa akiviongoza vikosi hivyo tangu July mwaka jana.Hata hivyo jenerali John Allen ataendelea kusimamia masuala ya Afghanistan kwasababu amekabidhiwa hatamu za uongozi wa juu wa vikosi vya NATO.

Kuteuliwa viongozi hao wawili wa kijeshi kunathibitisha uongozi wa Marekani katika kuushughulikia mzozo wa Afghanistan ulioangamiza maisha ya wanajeshi wake 2000 katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.

Anders Fogh Rasmussen Nato Brüssel Verteidigungsminister
Katibu mkuu wa jumuia ya kujihami ya NATO Anders Fogh RasmussenPicha: Reuters

Wakati wa mkutano huo mawaziri wa ulinzi wa jumuia ya kujihami ya NATO watabidi waidhinishe awamu ya kwanza ya mkakati wa kuwapatia "mafunzo ,ushauri na uungaji mkono" wanajeshi na polisi wa Afghanitan kuanzia amwaka 2015.

"Tume hii si ya mapigano" amekumbusha katibu mkuu wa jumuia ya NATO,Anders Fogh Rasmussen.

Inakadiriwa tume hiyo itakuwa na watu kati ya elfu 10 000 na elfu 20 kutoka jumuia ya kujihami ya NATO na mataifa sita mengine ambayo ni pamoja na Australia.

Kabla lengo hilo halijafikiwa jumuia ya kujihami ya NATO inatafuta ufumbuzi wa matatizo yanayozidi makali,ya mashambulio yanayfanywa na waafghanaistan wanaovaa sare za polisi au jeshi na kuwauwa wanajeshi wa nchi shirika.Wanajeshi 53 wameshapoteza maisha yao tangu mapema mwaka huu.

"Ni tatizo kubwa hili,maadui wanajaribu kuvuruga imani.Hawatafanikiwa..".amesisitiza katibu mkuu wa jumiia ya NATO Rasmussen.

Wakati huo huo waziri wa ulinzi wa Marekani Leon Panetta amezitolea mwito nchi shirika zichangie pia katika  kutuma wataalam kuwapatia mafunzo wanajeshi wa afghanistan akisema mchango wa Marekani "umepindukia."

Source News Feed: EMEA Picture Service ,Germany Picture Service German Defence Minister
Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Thomas de Maiziere akivitembelea vikosi vya KFOR huko KosovoPicha: Reuters

Katibu mkuu wa jumuia ya kujihami ya NATO Rasmussen amezungumzia pia umuhimu wa kuzidishwa idadi ya wanajeshi wa kulinda amani katika eneo la kaskazini la Kosovo ambako jamii ya wachache ya waserbia hawataki kutii amri ya serikali ya mjini Pristina.Ujerumani inayochangia wanajeshi wengi zaidi huko Kosovo (wanajeshi 1300) inapendelea ipunguzwe idadi ya wanajeshi walioko kusini ambako hali ni tulivu na kuimarishwa katika eneo la kaskazini.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Reuters/AFP/AP

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman