1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa Umoja wa Ulaya wakutana mjini Luxemburg

16 Oktoba 2006

Mvutano wa Uturuki na Cyprus wagubike mazungumzo ya Luxe,bourg

https://p.dw.com/p/CBIB
Picha: Fotomontage/AP Graphics/DW

Mvutano kati ya Umoja wa Ulaya na Uturuki kuhusu kisiwa cha Cyprus,kwa mujibu wa kamishna anaeshughulikia masuala ya kupanuliwa Umoja huo, Olli Rehn ,lazma upatiwe ufumbuzi hadi mwaka huu utakapomalizika.”Tungeweza katika kipindi cha wiki au miezi ijayo,kupata nafasi ya mwisho ambayo hatukuipata kwa muda mrefu kama si miaka.”Amesema hayo bwana Olli Rehn hii leo katika mkutano wa mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Umoja wa Ulaya uliohudhuriwa pia na waziri mwenzao wa Uturuki Abdallah Gül.Sambamba na mkutano huo ,mawaziri wa misaada ya maendeleo wamekutana mjini Luxemburg kuzungumzia miongoni mwa mengineyo juu ya kufunguliwa zaidi masoko ya Ulaya kwa bidhaa za nchi zinazoinukia.

Kamishna anaeshughulikia masuala ya kupanuliwa Umoja wa ulaya,Olli Rehn hajaridhika na mazungumzo pamoja na washirika wake wa Uturuki.Ingawa kimsingi mazungumzo ya kujiunga Uturuki na Umoja wa ulaya yamekua yakiendelea tangu mwaka sasa ,lakini hakuna bado maendeleo yoyote yaliyopatikana.

November nane ijayo bwana Olli Rehn atatoa ripoti yake ya mwaka ambayo haitazamiwi kutoa picha ya kutia moyo kuhusiana na mkondo wa mageuzi nchini Uturuki.

Mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Umoja wa Ulaya na waziri mwenzao wa Uturuki Abdallah Gül wanataka kuzungumzia zaidi suala la Cyprus.Uturuki inapinga kuziruhusu meli za Cyprus kutia nanga katika bandari zake au kuziachia ndege za kisiwa hicho kutuwa kama makubaliano ya umoja wa forodha ambayo Uturuki pia imetia saini,yanavyotaja.Kwa kufanya hivyo serikali ya mjini Ankara inataka kukwepa kuitambua jamhuri ya Cyprus –mwanachama wa Umoja wa ulaya tangu mwaka 2004.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Cyprus GEORGE Lillikas ametishia kutumia kura yake ya turufu kuzuwia mazungumzo yasiemndelezwe kati ya Umoja wa Ulaya na Uturuki.Umoja wa ulaya umeipa Uturuki muda wa hadi mwisho wa mwaka huu ifikirie la kufanya,anasema kamishna wa masuala ya kupanuliwa umoja wa Ulaya Olli Rehn:

“Huenda ikawa fursa ya mwisho,kwa muda mrefu pengine miaka,kwa suala la Cyprus,ndio maana pande zote zinazohusika zinabidi zijitolee ili kusaka ufumbuzi wa kisiasa wa mzozo wa Cyprus.”

Serikali ya Uturuki inataka kwa upande wake misaada ya fedha wapatiwe wakaazi wa kaskazini mwa Cyprus kama iliyoahidiwa na Umoja wa ulaya –jambo ambalo serikali ya jamhuri ya Cyprus-yaani jamii ya watu wenye asili ya kigiriki wanaoishi kusini mwa kisiwa hicho kilichogawika inapinga.Sehemu ya kaskazini inashikiliwa na uturuki tangu miaka 30 sasa.

Juhudi za Umoja wa mataifa za kukiunganisha upya kisiwa hicho zineshindwa kwa kura ya la ya waCyprus wenye asili ya kigiriki.

Mawaziri wa mambo ya nchi za nje walikutana pia na mawaziri wa misaada ya maendeleo kuzungumzia utaratibu mpya wa kupatiwa misaada nchi zinazoinukia.

Misaada ya serikali itazidishwa siku za mbele ili kupunguza kiu cha wahamiaji kinyume na sheria kutoka Afrika.Fedha hizo zinalengwa kugharimia miradi itakayoinua hali ya maisha ya waafrika nchini mwao.Waziri wa misaada ya maendeleo wa serikali kuu ya Ujerumani bibi Heidemarie Wieczoreck-Zeul anasema:

“Suala hili daima limekua likizungumziwa,na daima limekua likizungumziwa kwa mtazamo wa kujikinga.Na sasa,hata wale wanaotanguliza mbele suala la kinga,wamegundua kuna uwiano kati ya mambo haya mawili.Na mie ninawaambia,kawia ufike.”

Umoja wa Ulaya unajadiliana kwa sasa pamoja na mataifa yanayoinukia ya Afrika,Karibian na pacific njuu ya mkataba mpya wa ushirikiano utakaofungua njia ya kuzidi kufunguliwa masoko ya Umoja wa Ulaya kwa bidhaa kutoka nchi hizo za ACP.