1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wajadili mustakabali wa Kosovo

20 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cv0K

LJUBLJANA: Mawaziri wa Mambo ya Nje wa madola manne makuu ya Ulaya wamekutana na waziri mwenzao wa Slovenia nje ya Ljubljana kujadili mustakabali wa jimbo la Serbia la Kosovo.Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier na mawaziri wenzake wa Ufaransa,Uingereza na Italia walishiriki katika mazungumzo hayo lakini hakuna taarifa iliyotolewa.

Mgogoro wa Kosovo ni kipaumbele kwa Slovenia iliyoshika wadhifa wa rais wa Umoja wa Ulaya unaozunguka kila miezi sita.Viongozi wa jimbo la Kosovo lililo na wakaazi wengi wenye asili ya Kialbania wanataka kujitangazia uhuru wao upesi. Lakini Serbia imesema,kamwe haitokubali hatua ya Kosovo kujitoa kutoka Serbia.