1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo kuhusu hatima ya Kosovo yavunjika

29 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CUPF

Mazungumzo kuhusu hatima ya jimbo la Kosovo ambayo yamekuwa yakiendelea mjini Vienna nchini Austria yamevunjika.

Umoja wa Ulaya, Marekani na Urusi, zimewatolea mwito Waserbia na Walbania wasifanye machafuko kufuatia kuvunjia kwa mazungumzo ya hivi karibuni kuhusu hali ya baadaye ya jimbo la Kosovo.

Asilimia 90 ya Walbania wa Kosovo wanasisitiza uhuru kamili kutoka kwa Serbia, lakini serikali ya Serbia mjini Belgrade inataka jimbo hilo liwe na uhuru wa kujitawala lakini libaki kuwa chini yake.

Wapatanishi wa Umoja wa Mataifa watazuru Serbia na Kosovo Jumatatu wiki ijayo kwa mara ya mwisho kabla kuwasilisha ripoti yao kwa Umoja wa Mataifa hapo tarehe 10 mwezi ujao.

Kuna uwezekano mkubwa mkwamo kutokea katika baraza la usalama la umoja huo huku Urusi ikitarajiwa kuuzuia uamuzi ambao hautendana na idhini ya Serbia.

Viongozi wa Kosovo wamesema wanataka kutangaza uhuru haraka iwezekanavyo.