1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo kuhusu Sahara magharibi yaanza.

4 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CkQ0

Rabat. Mazungumzo kuhusiana na hali ya baadaye ya jimbo la Sahara magharibi yanaanza tena wiki ijayo na chama cha Polisario kinachopigania kujitenga kwa jimbo hilo kutoka Morocco kimeionya serikali hasimu ya Morocco kwamba kushindwa kupatikana kwa makubaliano ya msingi kunaweza kuzusha tena vita katika jimbo hilo.

Majadiliano hayo yanayodhaminiwa na umoja wa mataifa mjini New York ambayo yameanza siku ya Jumatatu, yatakuwa ya tatu yenye lengo la kumaliza mzozo huo wa kijimbo tangu pale Morocco na Polisario walipotoa mapendekezo kwa ajili ya jimbo hilo lenye utajiri mkubwa wa maliasili mwezi Aprili mwaka jana. Morocco ilichukua udhibiti wa jimbo hilo la Sahara magharibi mwaka 1975 baada ya mtawala wa kikoloni Hispania kujiondoa , na kusababisha mapigano ya chini kwa chini kwa ajili ya uhuru wa jimbo hilo ambayo yalimalizika mwaka 1991 wakati umoja wa mataifa uliweza kupatanisha na kupeleka jeshi la kulinda amani katika jimbo hilo.