1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya Kampala juu ya DRC yaonekana kugonga mwamba

MjahidA20 Desemba 2012

Huku raia wa Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo wakiwa na matumaini ya kupatikana amani nchini mwao kutokana na mazungumzo yanayofanyika nchini Uganda, sasa inaonekana matarajio yao huenda yakazimika

https://p.dw.com/p/1768L
Waasi wa M23
Waasi wa M23Picha: Phil Moore/AFP/Getty Images

Wakati raia wa Congo wakiendelea kutegea sikio yale yanayojitokeza katika mazungumzo yanayoendelea Kampala baina ya wajumbe wa serikali ya jamhuri ya kidemokrasi ya Congo na waasi wa M23, mazungumzo hayo bado yanaonekana kukabiliwa na mkwamo. Na ili kukwamua mazungumzo hayo, msuluhishi kwenye mazungumzo hayo waziri wa ulinzi wa Uganda Dr Crypius Kiyonga, yuko katika mchakato wakukutana na viongozi wa ujumbe wa M23, ili pande zote husika zikubali kurudi kwenye meza ya majadiliano.

Kwa mengi zaidi sikiliza ripoti ya mwandishi wetu John Kanyunyu aliyeko Kampala Uganda.

Mwandishi: John Kanyunyu

Mhariri:Yusuf Saumu