1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya kuunda serikali Berlin yaelekea mwisho

Sekione Kitojo
6 Februari 2018

Kansela Angela Merkel ameonya kuwa na mazungumzo yatakayohitaji maridhiano magumu wakati mazungumzo baina ya chama cha CDU na chama cha SPD kuunda serikali mpya nchini Ujerumani yakisua sua kwa siku ya pili leo Jumanne. 

https://p.dw.com/p/2sCXs
Deutschland Koalitionsverhandlungen von Union und SPD
Picha: Getty Images/AFP/J. Macdougall

Hali imefikia  hapo  baada  ya kushindwa  kupata  muafaka  wakati  muda  uliopangwa  kufanya hivyo  ukimalizika  mwishoni  mwa  juma. 

Mazungumzo  baina  ya  chama  cha  Christian Democratic Union CDU , cha  kansela  Angela  Merkel , washirika  wao  wa  chama cha Christian Social Union CSU  na  kile  cha  SPD yamekuwa yakifanyika  katika  makao  makuu  ya  chama  cha  DCU, baada  ya kufanya  mazungumzo  hayo  katika  makao  makuu  ya  SPD siku moja  iliyopita.

CDU-Parteizentrale Konrad-Adenauer-Haus
Makao makuu ya chama cha CDU mjini BerlinPicha: AFP/Getty Images/O. Andersen

Merkel  alisema  kabla  ya  kuanza  tena  mazungumzo  hayo kwamba  pande  zote  mbili zinahitaji kufikia maridhiano.  "Kila  mmoja wetu  bado  anahitajia  kufanya  maridhiano machungu. Niko  tayari kufanya  hivyo  iwapo  tutakuwa  na  uhakika  mwishowe   ambapo mambo  mazuri  yanashinda  uzito  yale  ambayo  si  mazuri," alisema Merkel.

"Tunaweza  tu  kusema  hatimaye  kwamba  kila  kitu  kimekubalika wakati  kila  kitu  kitakapokubalika  na  bado  tunahitaji  kukubaliana kuhusu  mada muhimu  sana. Afya, sheria za  kazi, kutegemewa kwetu  kimataifa. Baadhi  ya  mambo  haya  yanasikika  kuwa ni ya kitaalamu  zaidi  lakini  ni  kuhusiana  na ubora  ya  maisha  ya  watu na  kuwa  na  mafanikio  ya  kiuchumi.

Deutschland Koalitionsverhandlungen PK Angela Merkel
Kansela wa Ujerumani Angela MerkelPicha: Reuters/C. Mang

Kiongozi  wa  chama  cha  SPD Martin Schulz  alionesha  matumaini zaidi  wakati  akiingia  katika  mazungumzo  hayo. Nina  sababu  nzuri kufikiria tu  kwamba  tutamaliza  leo, nina  matumaini  katika  nia nzuri, kwa  matokeo mazuri  kwa  ajili  ya  nchi  yetu," Schulz alisema.

Ujerumani kuunda serikali imara

"Nafikiri  kwamba  leo  itakuwa  siku  ya  mwisho  ambayo  kutakuwa na  uamuzi  kuhusiana  na  iwapo  vyama  hivi  vitatu , CDU/CSU  na SPD vitaweza  kukamilisha  makubaliano  ya  kuunga  serikali  chini ya  msingi ambao serikali  imara  ya  Ujerumani  itaundwa. Na  si kingine  zaidi  ya  kwamba  tutaunda  serikali  imara  katika  moja ya taifa  kubwa  la  viwanda  duniani ambalo linaweza  kupambana  na changamoto  za  ndani  na  za  kimataifa.

Koalitionsverhandlungen zwischen Union und SPD
Mwenyekiti wa chama cha SPD Martin SchulzPicha: Getty Images/AFP/O. Andersen

Vyama  hivyo  vimefanikiwa  kufikia  makubaliano  katika  nyanja nyingi siku  ya  Jumapili  na  Jumatatu, ikiwa  ni  pamoja  na  nyumba , malipo  ya  uzeeni na  kuwa  na  mifumo  ya  kidigitali, lakini havikuweza  kukubaliana  kuhusu  afya, masoko  ya  kazi  na  sera za  mambo  ya  kigeni.

Masuala  muhimu  yanayorefusha  mazungumzo  ni  madai  ya chama  cha  SPD kufikishwa  mwisho  mfumo wenye ncha  mbili  wa afya, kupunguzwa   uwezo  wa  makampuni kuweka masharti  ya kufanyakazi na  mauzo  ya  nje  ya  silaha.

Deutschland PK Sondierungsgespräche in Berlin Merkel Seehofer und Schulz
Viongozi wa vyaam vinavyofanya majadiliano ya kuunda serikali. Horst Seehofer wa CSU(kushoto) Angela Merkel wa CDU (katikati) na Martin Schulz wa SPD (kulia)Picha: Reuters/F. Bensch

Iwapo vyama  hivyo vitafikia  makubaliano  leo, inatarajiwa  vitawasilisha  programu yao ya  kuunda  serikali na kugawana  nyadhifa za  serikali  ifikapo kesho Jumatano  licha  ya kiongozi  wa  chama  cha  SPD Martin Schulz  kutakiwa  na  wanachama  kutochukua  wadhifa  wowote katika  serikali  ya  Merkel  kwa  mujibu  wa  uchunguzi  wa  maoni uliofanyiwa  wanachama  wa  chama  cha  SPD.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / dpae

Mhariri: Idd Ssessanga