1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya Madagascar yaingia siku ya pili.

Mohamed Abdulrahman6 Agosti 2009

Mazungumzo ya kutafuta amani ya kudumu nchini Madagascar leo yameingia siku ya pili huko Maputo nchini Msumbiji.

https://p.dw.com/p/J4dI
Rais wa Zamani wa Madagascar Marc RavalomananaPicha: AP

Mahasimu wawili Rais wa Mpito nchini Madagascar Andry Rajoelina na rais wa zamani Marc Ravalomanana leo hii watajadili kiini cha mgogoro wa kisiasa nchini mwao.Mazungumzo hayo ya upatanishi ambayo unaingia siku ya pili mjini Maputo nchini Msumbiji, mazungumzo yake yanafanyika chini ya usimamizi wa Rais wa zamani wa Msumbiji, Joaquim Chissano.

Taarifa zilizotolewa na upande wa upatanishi zinasema kuwa siku ya kwanza ya mazungumzo yao ilikuwa kama kuweka mazingira sawa ya kuingia katika mjadala kamili leo hii.

Viongozi wanne wa kisiasa nchini Madagascar wakiwemo Didier Ratsiraka na Albert Zefy wanakutaka ana kwa ana kwa mara ya kwanza katika mjii huo mkuu wa Msumbiji ikiwa ni jitaha za kimtaifa za kurejesha amani nchini Madagascar.

Rajoelina aliingia madarakani huku akiungwa mkono na jeshi la nchi hiyo mwezi machi mwaka huu, ikiwa kipindu kifupi baada ya kutokea machafuko ambayo yalisababisha zaidi ya watu mia moja kupoteza maisha.

Madagaskar Unterstützer von Oppositionsführer Andry Rajoelina feiern
Rais wa Mpito wa Madagascar Andry Rajoelina akisindikizwa na jeshi la nchi hiyoPicha: AP

Siku ya kwanza,ya ufunguzi wa mkutano huo jana likuwa ni kukutana kupeana mikono ya heri baada ya vuta nikuvute iliyokea nchini mwao.

Rais Joaquim Chissano mwenyewe alinukuliwa akisema``Umuhimu wa suala hili mataifa yote yaneelewa, kwa wahusika wote na kwa maslahi ya taifa,imeelewekwa kuwa nchi zote hazipendezwi na machafuko,tupo hapa leo kuyamaliza na kusuluhisha.``

Mmoja kati ya Waratibu wa mkutano huo kutoka Taasisi ya Kimataifa ya nchi zinazozungumza Kifaransa Edem Kodjo amesema washiriki wote wameonekana kuwa katika hali nzuri ya kushiriki vyema mjadala huo na kuheshimiana.

Katika mkutano wake na Msuluhishi ,Ravalomanana ameahidi kuhakikisha katiba ya Madagascar inafuatwa na kutoa wito wa utawala wa sheria ili kuanza mapatano.

Alisitiza kuheshimiwa kwa demokrasia ya nchi hiyo kwa namna yeyote pamoja na kushirikiana pamoja kutafuta suluhu ya mgogoro nchini mwao.

Katika kauli yake hiyo mbele ya msuluhishi,Rais wa Zamani wa Msumbiji,Ravalomanana ameongeza kuwa maslahi ya Wamadagascar yatangulizwe mbele kuliko wao wote.

Nae Andry Rajoelina akizungumza na Waandishi wa Habari kabla ya kuwasili Maputo alisema lengo lake la kuudhuria mkutano huo ni kumaliza mgogoro na kustawisha amani nchini Madagascar.

Aidha amesisitiza kuwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo utarajiwe 2010 na kwamba utafanyika kwa mazingira salama na amani kabisa.

Timu ya Wasuluhishi inajuimisha Wajumbe kutoka Umoja wa Afrika,Umoja wa Mataifa,Jumuia ya Kimataifa ya nchi zinazozungumza Kifaransa na Jumuiya ya Maendeleo ya nchi zilizo Kusini mwa Afrika-SADC.

Mwandishi:Sudi Mnette/AFP

Mhariri:M.Abdul-Rahman