1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya nyuklia ya Iran yaendelea

7 Julai 2015

Wakati kumekuwa na matarajio madogo ya kufikia makubaliano kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran katika mazungumzo ya Vienna Iran imesema hatua imeipigwa katika mchakato mzima wa mazungumo hayo.

https://p.dw.com/p/1Ftw1
Österreich Palais Coburg Gespräche E3+3
Wajumbe wa mkutano wa nyuklia wa Iran mjini ViennaPicha: picture-alliance/dpa/G. Hochmuth

Taarifa hiyo inatolewa wakati tarehe ya mwisho ya makubaliano ya mpango wa nyuklia kati ya Iran na mataifa mataifa makubwa yenye nguvu duniani yenye kuitwa kwa kifupi P5+1( Uingereza, China, Ufaransa, Urusi, Marekani na Ujerumani) hii leo inaonekana kama haitofikiwa .

Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa hayo walifanya mazungumzo hadi usiku wa manane jana huku kukiwa na masuala magumu ambayo yanasalia kutatuliwa kabla ya kufikia makubaliano hayo muhimu yanayotarajiwa kuumaliza mzozo huo wa kinyuklia ambao umedumu kwa takriban miaka 13.

Wataalamu wa nyuklia nchini Iran

Kwa upande mwengine ziara ya masaa 24 ya Jumatatu ya wataalamu kutoka Shirika la Nguvu ya Atomiki (IAEA), ilifuatiwa na nyingine kama hiyo ya juma lililopita ya mkuu wa shirika hilo Yukiya Amano, lakini hakuna matokeo ya wazi yaliofikiwa.

IAEA Direktor Yukiya Amano
Mkuu wa Shirika la Nguvu za Atomik Duniani Yukiya AmanoPicha: Reuters/L. Foeger

Akinukuliwa na Shirika la Habari la Iran (IRNA), msemaji Shirika la Nguvu za Atomic nchini Iran, Behrouz Kamalvand, alisema kwamba hatua zimepigwa pasipo kutoa maelezo zaidi kuhusi mijadala ya hivi karibuni. Alisema " Iran na IAEA zimepiga hatua kubwa katika kutatua tofauti zilizopo katika kufikia makubaliano ya masuala ya msingi na kushirikiana kwa wakati.

Nia ya dhati ya kutatua mzozo

Kamalvandi aliuelezea mkutoano wa Jumatatu kama "mkutano wenye kujenga zaidi na kuonesha maendeleo". Na kuongeza kwamba ujio wa pili wa IAEA unaonesha nia ya dhati kwa pande zote mbili katika kuongeza ushirikiano.

Shirika IAEA mpaka 2003 limekuwa likituhumu Iran kuendeleza utengenezaji silaha za nyuklia. Shirika hilo linaomba uwezekano wa kuwafikia wanasayansi ambao wanaweza kuwa wamehusika na mpango huo, pamoja na nyaraka na vilevile maeneo ambayo majaribio hayo yamekuwa yakifanyika.

Iran imekanusha tuhuma zote na kiongozi mkuu Ayatollah Ali Khamenei, katika hotuba yake ya Juni 23 aliondoa kabisa uwezekano wa wachunguzi kufika katika maeneo ya kijeshi au ya wanasayansi wa nyuklia.

Mwandishi: Sudi Mnette AFPE

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman