1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya upatanishi Mashiriki ya Kati kuanza tena

10 Machi 2012

Kundi la pande nne la wapatanishi wa mzozo wa Mashariki ya Kati - Marekani, Urusi, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya, litakutana Jumatatu kujadili mpango wa amani uliokwama baina ya Israel na Palestina.

https://p.dw.com/p/14Ib4
epa02928215 US President Barack Obama (R) met with Israeli Prime Minister Benjamin Netanyahu (L) on the sideline of the 66th session of the United Nations General Assembly at United Nations headquarters in New York, New York, USA, 21 September 2011. Reports on 21 September 2011 state that Palestinian Authority President Mahmoud Abbas is to present the Palestinian request to become the 194th member of the UN on 23 September, after he addresses the General Assembly. The bid has to be approved by the 15-member Security Council, where it will almost certainly meet with a veto by the US. EPA/AARON SHOWALTER / POOL
Barack Obama und Benjamin NetanyahuPicha: picture-alliance/dpa

Umoja wa Mataifa umesema jana Ijumaa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton na Waziri wa Mambo ya nchi za Kigeni wa Urusi Sergei Lavrov watakutana katika makao mkuu wa Umoja wa Mataifa kabla ya kikao maalum cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu wimbi la mageuzi katika ulimwengu wa Kiarabu. Washirika wengine wa majadiliano hayo - Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton na mjumbe maalum wa kundi hilo Tony Blair watachangia kupitia njia ya video.

Wajumbe wa Umoja wa Mataifa wamesema Urusi imeanza kushinikiza kuandaliwa kwa mkutano huo wa pande nne. Haikubainika ikiwa kundi hilo lilipanga kutoa taarifa ili kuhimiza kurejelewa mazungumzo hayo baina ya Waisrael na Wapalestina, suala ambalo limezungukwa na mjadala baina ya Israel na Marekani kuhusu uwezekano wa shambulizi la kijeshi dhidi ya Iran kutokana na mpango wake wa nyuklia.

Ulimwengu hauskii kilio cha Palestina

Huku wakikumbwa na mizozano ya kindani, Wapalestina wamejizatiti kupaza sauti zao zisikike katika miezi ya hivi karibuni. Macho ya ulimwengu yameangazia uchaguzi wa rais nchini Marekani, machafuko yanayoshuhudiwa nchini Syria na mpango wa nyuklia wa Iran.

Palestina inataka kutambuliwa na Umoja wa Mataifa kama taifa huru
Palestina inataka kutambuliwa na Umoja wa Mataifa kama taifa huruPicha: dapd

Ban Ki Moon alisema mjini Jerusalem mwezi jana kuwa Israel na Wapelestina wanaishiwa muda wa kutatua mzozo wao na wanapaswa kulipa kipau mbele suala la kurejelea mazungumzo.

Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas, analo sharti la mazungumzo hayo, anataka Israel ikubali kuundwa wka taifa la Palestina kwenye ardhi yake yote iliyochukuliwa katika vita vya Mashariki ya Kati vya mwaka ya 1967.

Rais wa Israel Benjamin Netanyahu amekataa kukubali ombi hilo na amepuuza masharti ya Wapalestina ya kusitisha shughuli za ujenzi wa makaazi katika ardhi ambayo Wapalestina wanataka kuwa taifa lao.

Mwandishi: Bruce Amani/Reuters

Mhariri: Sekione kitojo